Habari za Simba SC
Habari za michezo

ISHU YA MGUNDA KURUDI SIMBA …UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…KAPEWA MASHARTI ‘KIBAO’…

admin November 18, 2023 4:30 pm

Kocha kipenzi cha mashabiki wa soka nchini, Juma Mgunda amerejea ulingoni baada ya kupewa mikoba ya kuinoa timu ya soka wanawake ya Simba, Simba Queens, kwa msimu wa 2023/2024 utakaoanza hivi karibuni akisaidiana na Mussa Hassan Mgosi.

Mgunda aliyewahi kuzinoa Coastal Union, Taifa Stars na Simba kwa mafanikio kabla ya kuachia ngazi kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi ataanza kuonekana kwenye benchi la Simba Queens kuanzia mwishoni mwa mwezi huu katika ufunguzi wa Ligi Kuu Wanawake (WPL).

Kati ya vipengele alivyonavyo Mgunda katika majukumu yake mapya ni kurejesha ubingwa kwa timu hiyo uliochukuliwa na JKT Queens msimu uliopita ikiwanyang’anya Wekundu hao waliokuwa wanaushikilia kwa misimu mitatu mfululizo.

Tayari Mgunda amejiunga na timu hiyo na ameanza maandalizi ya msimu mpya ikiwamo kufanya usajili ambao hadi sasa timu imemtambulisha winga Mkongomani Diakiese Issabelle kutoka FC Feminin na wengine watafuata.

SAUTI YA MASHABIKI SIMBA YAFIKIWA…TRY AGAIN AKUBALI YAISHE ….ANYOOSHA MIKONO JUU… HAWA HAPA MASTAA 10 WALIOKIWASHA KISAWASAWA NA MAN UNITED…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply