Habari za Simba leo
Habari za michezo

HII SASA NDO INAITWA SIMBA NA MKATABA WA BALEKE……. NI UMAFIA TU

Staff Desk November 20, 2023 6:12 am

Klabu ya Simba inaelezwa ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Jean Othos Baleke kwa kumpa mkataba wa kudumu klabuni hapo.

Inafahamika kua mshambuliaji Jean Baleke alikua kwa mkopo klabuni hapo akitokea Tp Mazembe ya nchini Congo, Lakini Simba wanaelezwa wako mwishoni kumalizana na mshambuliaji huyo na kumpa mkataba wa kudumu.

Mazungumzo baina ya Wekundu wa Msimbazi na Tp Mazembe yameenda vizuri na ndio sababu ya klabu hiyo kufikia katika hatua nzuri na mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Congo.

Jean Baleke amekua na kiwango bora sana ndani ya klabu ya Simba tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha dogo la mwezi Januari msimu uliomalizika, Jambo lililowavutia kutaka kumpa mkataba wa kudumu aendelee kusalia kwenye viunga vya Msimbazi.

Klabu ya Simba inahitaji kufanya maboresho klabuni hapo katika dirisha dogo la mwezi Januari, Hivo klabu inahitaji kuwapa mikataba wachezaji wake ambao wanamaliza muda wao klabuni lakini pia kuongeza wa nje ya klabu hiyo.

SIMBA SASA NI MTUNISIA MANARA AKABIDHIWA KIPAZA SIKU YA MCHEZO WA MOROCCO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply