Ikiwa imepita miezi kadhaa Wanayanga wakiwa na kumbukumbu mbaya baada ya kupoteza Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya USM Alger iliyokuwa chini ya Kocha Abdelhak Benchikha, sasa mbabe huyo ametua kwa watani wao Simba akisaini mkataba wa miaka miwili.
Simba imethibitisha kumchukua kocha huyo ambaye atakuwa mrithi wa mikoba ya Robertinho ambaye aliacha kibarua cha kuinoa Simba Novemba 07, 2023.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu vya ndani, Benchikha huenda akalipwa mshahara kati ya Milioni 30-45 kwa mwezi , atapewa bonasi ya milioni 40 endapo Simba watafika nusu fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Aidha, bonasi nyingine , ni pamoja na Tsh Laki tano kwa kila mechi ya ndani (Ligi Kuu ya NBC na Kombe la FA) atakayoshinda, na atapewa Milioni moja mpaka mbili kwa kila mechi za kimataifa atakayashinda.
Mbali na Hivyo, Benchikha atapewa Nyumba ya kitajiri maeneo ya ‘ushuani’, atapewa gari la kisasa la kutumia likiwa full oil kwa kipindi chote atakachokuwa kocha wa Simba, atapewa vocha ya laki tano kwa matumizi yake ya simu.
CV YA KOCHA MPYA SIMBA
Name: Abdelhak Benchikha
22 November 1963 (age 60)
Place of birth
Bordj Bou Arréridj, Algeria
Timu alizowahi kufundisha ni
CR Belouizdad
MC Alger
Algeria U23
CA Bordj Bou Arréridj
CR Belouizdad
Umm Salal
ES Zarzis
Club Africain
Algeria A’ / Algeria U23
Algeria
MC Alger
Club Africain
Difaâ El Jadidi
Raja Casablanca
Al-Ittihad Kalba
IR Tanger
Raja Casablanca
Moghreb Tétouan
ES Sétif
Al-Ittihad Tripoli
Mouloudia Oujda
DH El Jadida
RS Berkane
USM Alger
Nawashukuru sana wana simba lakin timu yet shida niwachezaji wamechoka sana wana takiwa wengineo wapewe mda wakupumzika
Kabisa ni kweli wachezaji wa simba hawajitumi na mpira hauna kasi kama tunavyotamani kuona na kingine wanawatoa wachezaji ambao wako vizuri kidogo,wanaleta wachezaji ambao ni empty kabisa,ko kwa maana hiyo simba ahipigi hatua bali ni kubaki tulipo au kurudi nyuma kabisa