Klabu ya Yanga ‘Wananchi’ wameianza hatua ya makundi kwa kichapo cha mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Makundi baada ya kukubali kufungwa na CRBelouizdadugenini nchini Algeria.
Hii ni sawa na msimu uliopita kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho ambapo walianza mchezo wa kwanza ugenini kwa kichapo dhidi ya US MONASTIR ya Tunisia.
Mchambuzi wa Efm radio Jemedari Said Kazumari amesema;
“Sio matokeo mazuri, lakini haikuwa performance mbaya saaana, mabao yamefungwa kwenye muda ambao umakinifu huwa mdogo kitaalamu kwa wachezaji. Dakika 10 za mwanzo wa mchezo, dakika chache kabla ya mapumziko na dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho.
“Kwa muda mrefu wa mchezo Yanga wamekuwa na very impressive performance kwa wachezaji mmoja mmoja na kwa timu, bado kuna mechi 5 za kucheza nafasi ipo kubwa.”
Katika hatua nyingine, Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amedai kuwa wao walimiliki zaidi mpira lakini wapinzani wao, kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika, CR Belouzdad wakamiliki matokeo.
“Tumemiliki mchezo, wenzetu wakamiliki matokeo, It’s Football..Hongera kwao. Hii imekwisha Kituo kinachofuata ni Benjamin Mkapa Daima mbele Nyuma Mwiko,” amesema Ally Kamwe baada ya Yanga kupata kichapo cha goli 3-0.
Desemba 2, Yanga atakuwa na kibaura kingine dhidi ya Al Ahly ya Misri katika Dimba la Mkapa.