Habari za Simba
Habari za michezo

MASTAA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU UGAMVI UNAOENDELEA KWENYE KLABU HIYO

Staff Desk November 27, 2023 11:37 am

Nyota wa Zambia anayechezea Simba SC, Clatous Chama amesema anakiri kwamba hawakucheza vizuri kwenye michezo mitatu iliyopita lakini si kwamba kuna ugomvi ndani ya timu.

Chama amesema, kwa sasa Simba hawatakiwi kunyosheana vidole na badala yake waungane, waisapoti timu ili waweze kurudi kwenye matokeo yao ya kuwapa furaha Wana-Simba.

“Msimu uliopita Champion League tulianza vibaya, tulipoteza dhidi ya Horoya, tukaja tukapoteza dhidi ya Raja lakini baadaye tuliamka na kupata matokeo yaliyotuwezesha kuvuka kwenda hatua iliyofata ya Robo Fainali,” alisema Chama.

Simba wamekuwa na wakati mbaya baada ya kupoteza michezo mitatu iliyopita kwa mmoja kufungwa na Yanga, miwili sare dhidi ya Namungo FC (1-1) na dhidi ya ASCE Mimosas (1-1).

KISA SAFARI YA ZANZIBAR ALLY KAMWE AMPIGA KIJEMBE FEI TOTO YOTE TISA….TATIZO LA SIMBA MPAKA KUFIKIA HAPO WALIPO..UKWELI WOTE USIOSEMWA HUU HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply