Home Habari za michezo SIMBA vs ASEC MIMOSAS…,MBIVU NA MBICHI HIZI HAPA….,MASTAA HAWA KUKOSEKANIKA…..

SIMBA vs ASEC MIMOSAS…,MBIVU NA MBICHI HIZI HAPA….,MASTAA HAWA KUKOSEKANIKA…..

Habari za Simba

SIMBA leo inashuka dimbani kumenyana na Asec Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo wa kundi B, Simba wanashuka wakiwakaribisha Asec Mimosas kwenye dimba la nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 16: 00 alasiri. kimachovutia zaidi ni kiwango cha timu hiyo kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Katika mchezo wa mwisho wa timu hizo katika uwanja wa Benjamin Mkapa Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho hatua makundi

Kwa msimu huo walicheza mara mbili kila mmoja ameshinda mechi moja, kupoteza moja, huku Simba wakiwa na wastani wa kufunga 1.5 huku Asec Mimosas akiwa 2 . Kwa upande wa kuruhusu magoli Wekundu hao wa Msimbazi wakiwa na 2 na mpinzani wake akiwa na 1.5

Simba ambao wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika michezo nane waliyocheza wameshinda sita, sare moja na wamepoteza moja wakikusanya alama nane.

Asec Mimosas ambao wanaongoza ligi ya Ivory Coast wakicheza michezo 11, wameshinda saba, sare moja na wamepoteza mechi tatu wakiwa na alama 22.

Kuelekea mechi ya leo kaimu kocha mkuu wa Simba, Daniel Cadena amesema wamefanya kazi katika kile eneo ikiweo kiakili, kimwili na kiufundI na kikosi kipo tayari kwa mchezo wao wa leo.

Amesema katika mchezo huo atakosa huduma ya nyota wake wawili akiwemo kiungo wake Clatous Chama ambaye amechelewa kujiunga na timua akitokea kwenye majukumu ya timu ya Taifa Zambia na Kipa wake Aishi Manula alipata jeraha dogo katika mchezo uliopita na Niger.

“Hatukuwa na matokeo mazuri mechi iliyopita tukapata muda wa kujiandaa na kubadilisha vitu vingi ninaimani tutapata matokeo mazuri kulingana na maandali tuliyofanya.

Asec Mimosas tumewaona na tutacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikusha tunafanikiwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kuibuka na ushindi kesho (leo),” amesema Cadena.

Amewataka mashabiki kujitokea kwa wingi kwa sababu nguvu yao inaongeza kuleta ushindani na anaimani kubwa ya kufanya vizuri na kupata ushindi katika mchezo huo wa leo.

Naye mwakilishi wa wachezaji wa Simba, Che Malone Fondoh amesema hawana cha kuahidi zaidi ya kwenda kupambana na kutafuta ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Asec Mimosas.

Amesema wanarudi na njia yao ya kuhakikisha wanapambana kutafuta matokeo mazuri kwa kufuata maelekezo waliyopewa na benchi la ufundi kwa ajili ya kusaka ushindi.

“Tumejiandaa vizuri kikubwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kutusapoti, maandalizi yameenda vizuri matarajio yetu ni kushinda katika mchezo wetu juu,” amesema Che Malone.

Kocha Mkuu wa Asec Mimosas, Jullien Chevaller, amesema anafuraha ya kufika salama na kufukia nafasi ya kucheza hatua ya makundi ambayo anaima kuna timu bora ambazo hazijafikia katika hatua wanayocheza.

“Wamekuwa na uzoefu wa muda mrefu na anaimani ya kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Simba na kupata matokeo mazuri ikiwa ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi,” amesema Jullien.

Amesema muhimu timu ilipotia changamoto nyingi ikiwemo Covid 19 kwa kushinda kushirikia vizuri na sasa wako vizuri na wamekuja kutafuta matokeo mazuri.

Ameongeza kuwa hakuwa na muhimu kupata taarifa kupitia wachezaji ambao walikuwepo msimu uliopita katika kikosi chake na sasa wako Yanga bali alitumia mechi za Simba na kucheza kwa mujibu ambao watacheza wapinzani wao katika mchezo wa leo.

“Tunasahau matokeo ya mwisho na hayapo katika vichwa vyetu kwa sababu kwa sasa tunaangalia kilichokuwepo mbele yetu ni kutafuta ushindi dhidi ya Simba,” amesema Jullien.

Nahodha wa Asec Mimosas, Essie Aka amesema wamejiandaa vizuri na hakuna cha ziada walichokuja nacho zaidi ya kucheza na Simba na kupata matokeo chanya.

Amesema wameshiriki mashindano na timu kukutana na timu nyingi wamekuwa na uzoefu mkubwa na wamejiandaa vizuri na sasa wanasubiri muda wa uwanjani ambapo dakika 90 zitaongea.

“Hatuangalii Simba wamefanya nini katika mechi zilizopita na sasa wanaangalia wanaenda kufanya nini katika mchezo wao kesho (leo) kuhakikisha wanafanya vizuri,” amesema Aka.

SOMA NA HII  WAKATI MAWAZO YA SIMBA YAKIWA KWA WASAUZI KWANZA...YANGA WAIBUKA NA KUTOA MSIMAMO WAO...