Habari za Simba leo
Habari za michezo

AHMED ALLY ASEMA HAYA KUHUSU WYDAD SIO POA

Staff Desk December 4, 2023 3:46 pm

Afisa Habari na Mawasiliano wa ‘klabu’ ya #SimbaSC, #AhmedAlly amedai kuwa ‘klabu’ ya Wydad ni mnyama mkali aliyesinzia hivyo wanatakiwa kujiandaa kukabiliana nao katika ‘mechi’ ya ‘ligi’ ya mabingwa #Afrika inayotarajiwa kuchezwa Desemba 9.

Ahmed ameyasema hayo kupitia ukurasa wa Instagram ameandika ujumbe kuwa kikosi chao kinarejea kambini leo kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya ‘klabu’ ya Waydad Casablanca.

Hata hivyo ameeleza kuwa mpinzani wao japo amepoteza ‘mechi’ mbili lakini hiyo haiwapi nafasi ya kwenda bila kujiandaa kwani ‘timu’ hiyo ni kama mnyama mkali aliyesinzia na huwezi jua ataamka saa ngapi na ataamkia kwa nani.

Hivyo wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya wapinzani wao kwa dhumuni la kuondoka na ushindi na kuongeza point katika mashindano hayo.

Simba iliyo nafasi ya tatu kwenye kundi B, inatarajia kuwa uwanjani siku ya Jumamosi Desemba 9, kwenye mchezo wa tatu wa awamu ya kwanza ya hatua ya makundi dhidi ya Wydad ya Morocco.

JICHO LA KIUFUNDI ZAIDI…..YANGA vs AL AHLY NGOMA ILIFELIA HAPA…GAMONDI NI CHANZO..? SIO SIMBA, YANGA MAMBO NI MAGUMU STORI KAMILI IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply