Habari za michezo
ALLY KAMWE AINGIA UPEPO MBELE YA MADEAMA BAADA YA KUSHINDWA KUTAMBA DHIDI YA AL AHLY
Staff Desk
December 5, 2023
11:56 am
Klabu ya Young Africans imesafiri kuelekea nchini Ghana alfajiri ya leo kwa ajili ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Medeama.
Afisa habari wa klabu hiyo Ali Kamwe amesema wanatarajia kukutana na upinzani mgumu katika mchezo huo na hautakuwa mchezo rahisi.
Ali Kamwe amewaomba wadau na mashabiki wa soka nchini kuiombea timu yao na panapo majaaliwa watarejea na ushindi nchini.
Yanga ipo mkiani mwa kundi D ikiwa na alama moja pekee katika michezo miwili iliyocheza.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.