Home Habari za michezo NJIA YA YANGA KUTOBOA MAKUNDI CAF HII HAPA….WAKISHINDWA NA HII NDIO BASI...

NJIA YA YANGA KUTOBOA MAKUNDI CAF HII HAPA….WAKISHINDWA NA HII NDIO BASI TENA…

Habari za Yanga

Ukitazama msimamo wa kundi D lenye timu za Al Ahly, CR Belauizdad, Yanga na Madema na ukafanya tathmini kwa kutumia hesabu za kimpira, hutopingana nami kuwa Yanga wana nafasi kubwa ya kusonga hatua ya robo fainali.

Kivipi?

Mechi zinazofuata ambazo ni za mzunguko wa 3, Yanga watakuwa ugenini dhidi ya Madeama, wakati huo Al Ahly watakuwa nyumbani dhidi ya CR Belauizdad.

Kutokana na matokeo ya michezo miwili iliyopita, ni wazi kuwa iwe isiwe ni lazima Yanga wahakikishe wanapata point 3 ugenini. Na wakishindwa kabisa basi angalau wapate point 1.

Kama watatoa suluhu watakuwa na point 2, wakiendelea kushika mkia kwenye kundi lao. Wakati huo Belauizdad wakiwa ugenini dhidi ya National Al Ahl na wakapoteza, basi msimamo wa kundi D utaendelea kuongozwa na;-

1. Al Ahly (7)
2. Madeama (4)
3. Belausdad (3)
4. Yanga (2).

Kwenye mzunguko wa 4, Yanga watawakaribisha Madeama kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa. Na Belauisdad watakuwa nyumbani dhidi ya Al Ahly. Kwenye mchezo huu naziona point 3 za wazi kwa Yanga, huku Belauisdad wakigawana point na Al Ahly.

Hapo msimamo utakuwa;-
1. Al Ahly (8)
2. Yanga (5)
3. Belauizdad (4)
4. Madeama (4)

Mzunguko wa 5 utawakutanisha Yanga vs Belauizdad kwenye dimba la Benjamin Mkapa, wakati Al Ahly watakuwa ugenini dhidi ya Mediama.

Hapa kwa Mkapa, Yanga hawatotakiwa kupoteza tena mchezo. Watatakiwa kupambana na wahakikishe wanawafunga Belauizdad huku Al Ahly nao wakimchapa Madeama nyumbani kwake.

Hapo msimamo wa kundi D utaendelea kuongozwa na;-
1. Al Ahly (11)
2. Yanga (8)
3. Belauizdad (4)
4. Madeama (4)

Mzunguko wa 6 ambao ndio utakuwa wa mechi za mwisho. Yanga dhidi ya Al Ahly ugenini, Belauizdad dhidi ya Mediama nyumbani.

Hizi zitakuwa mechi za kukamilisha ratiba tu, kwani hata ikitokea Yanga wakapoteza dhidi ya Al Ahly, na Belauizdad wakashinda dhidi ya Madeama bado msimo wa kundi D utabaki vilevile.

1. Al Ahly (14) ✅️
2. Yanga (8) ✅️
3. Belauizdad (7) ❌
4. Madeama (4) ❌

Kumbuka hii ni imagination tu kulingana na hesabu za kimpira. Mwisho wa siku, dakika 90 za mchezo ndio zitakazoamua nani atasonga mbele na nani atabaki?!

Kwenye soka lolote linaweza kutokea.

SOMA NA HII  KISA YANGA KUWA NA POINT 13 CAF....JEMEDARI 'MCHAMBA' MANARA KWA HILI...AMUITA MPUUZI...