Habari za Simba
Habari za michezo

KAPOMBE ATULIZA MZUKA SIMBA…AFUNGUKA WALICHOFANYIWA NA BENCHIKHA….

admin December 5, 2023 8:11 pm

Beki wa Simba SC Shomari Kapombe amewaambia mashabiki wa klabu yake, wasiwe na wasiwasi kwani wanayo nafasi ya kufuzu hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika.

Kapombe ametoa kauli hiyo leo mchana alipokuwa anaondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kupambana na Wydad Casablanca.

“Tunazo mechi nyingi bado, tunayo nafasi ya kusahihisha makosa yetu na kufanya vizuri. Kikubwa mwalimu amefanyia kazi hasa eneo la ulinzi na ushambuliaji, nina imani tutafanya vizuri,” alisema Shomari.

Simba itapepetana na Wydad Jumamosi hii Desemba 9,2023. Simba wana alama 2 kwenye makundi, Wydad hana alama yoyote.

Katika hatua nyingine, Beki wa kulia wa Simba SC, Shomari Kapombe ameweka wazi kuwa siri kubwa iliyowafanya wachezaji wa Simba kuonesha kiwango kizuri ni maneno waliyopewa na mwali wao mpya Benchikha.

Kapombe amesema, mwalimu alizungumza na mchezaji mmoja mmoja na kumuambia kuwa anahitaji kila mtu aipambanie timu na hicho ndicho kilicholeta mabadiliko kwenye mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy.

“Mwalimu alituambia anahitaji tujitume, kweli tulifanya hivyo na tukafanikiwa lakini hatukuweza kupata bahati ya kufunga,” alisema Kapombe.

MZEE WA JAMBIA AIKATAA YANGA KIMATAIFA….”WAKIFUZU ROBO FAINAL ITAKUWA BAHATI KWAO”… NJIA YA YANGA KUTOBOA MAKUNDI CAF HII HAPA….WAKISHINDWA NA HII NDIO BASI TENA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply