Mbili Za Ligi Kuu Zamuwania Ladaki Chasambi
KIUNGO wa Simba, Ladaki Chasambi huenda akaitumikia Mashujaa au Pamba Jiji kwa mkopo msimu ujao ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara baada ya kushindwa kupata namba kikosini hapo.
Taarifa zinaeleza uongozi wa mchezaji huyo ulianza kutazama uwezekano wa kumrejesha Mtibwa Sugar, lakini baada ya klabu hiyo kushuka daraja, sasa unaelekeza nguvu Mashujaa au Pamba Jiji ambazo zimeonyesha utayari wa kumpokea.
Chasambi amekuwa akipata ushindani mkubwa wa nafasi ndani ya Simba, hasa baada ya ujio wa kocha Steve Barker, ambapo analazimika kuwania namba na viungo Libase Gueye, Elie Mpanzu na Inno Loemba ambao wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri na kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.
“Tunatamani acheze na arudi kwenye kiwango chake, kukaa benchi muda mrefu kumemrudisha nyuma hivyo tumeona ni sahihi yeye kwenda kwa mkopo acheze angalau,” kilisema chanzo hicho na kuongeza.