Habari za Simba leo
Habari za michezo

TUTAKACHOMFANYA WYDAD ATAJUTA KUJA….. AHMED ALLY

Staff Desk December 13, 2023 1:56 pm

Simba SC, wamesema watahakikisha wanamfunga kwa idadi kubwa ya magoli Wydad katika mechi yao ya nne ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika Desemba 19, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Kauli hiyo ya kishujaa imetolewa na Semaji la CAF, Ahmed Ally alipokuwa kwenye uwanja wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Simba Queens na JKT Tanzania.

Kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa ya Ngao ya Jamii, Simba Queens aliibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 5-4.

“Wydad inabidi achakae vibaya mnoo, achakae kwa namna ambayo hajawahi kuchakaa…. Safari hii akija Benjamin Mkapa sio afungwe kagoli kamoja afungwe kwa namna ambayo hajawahi kufungwa, tutamfanya vibaya Wydad, kikubwa wanasimba mjiandae kwenda uwanjani,” alisema Ahmed.

SIMBA KUWATUMIA KAGERA SUGAR KAMA DARAJA LIGI KUU, UONGOZI WAFUNGUKA HAYA UNAAMBIWA MASTAA HAWA WATATU TU NDIO WAMEMKOSHA BENCHIKHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply