Home Habari za michezo BENCHIKA AANZA KUONA MWANGA SIMBA….KINA INONGA NA WENZAKE WAKIONA CHA MOTO..

BENCHIKA AANZA KUONA MWANGA SIMBA….KINA INONGA NA WENZAKE WAKIONA CHA MOTO..

Habari za Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ameanza kufanikiwa kwa asilimia 70 kwa kuimarisha safu yake ulinzi baada ya mchezo wa juzi kutoruhusu bao la kufungwa tofauti na michezo iliyopita ambapo wameruhusu bao kila mechi.

Amesema anawapongeza wachezaji wake hasa safu ya ulinzi kwa kufanikiwa kupata ‘Clean Sheet ‘ na kupata ushindi wa mabao 3 -0 dhidi ya Kagera Sugar ni sehemu ya mchezo muhimu kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca

Kauli hiyo aliizungumza mara baada ya dakika 90 kukamilika mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar, Simba ikifanikiwa kuvuna alma tatu muhimu, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Benchikha amesema uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi lakini hata hivyo amefurahi kwa ushindi huo mnono na wachezaji kufanya kile alichowapa kwenye uwanja wa mazoezi.

Ameeleza kuwa Kagera ni timu nzuri na walitoa ushindani mkubwa lakini wao walikuwa bora katika kila eneo ikiwemo safu ya ulinzi ambayo hawajaruhusu wapinzani wao kupata bao na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Tumecheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu, tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi, Kagera ni timu nzuri wanacheza soka safi na walitupa ushindani mkubwa ingawa sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi,” amesema Benchikha.

Ameongeza kuwa ameridhishwa na jinsi ya safu yake ya ulinzi kuwa makini na anaimani kubwa kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablanca watafanya vizuri na kuibuka na ushindi ambao kwao ni muhimu.

“Baada ya mechi hii tunaenda kucheza mechi ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, kwetu ni fainali kwa sababu tunahitaji ushindi, tunarudi uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu yetu,” amesema Benchikha.

Amewaita mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Jumanne kushuhudia timu yao kwa sababu wamefanya kuwa maandalizi mazuri na kuhitaji kupata ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kwenda robo fainali .

Naye kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema mpira mchezo wa makosa, amewapongeza Simba walicheza vizuri na walistahili kupata ushindi huu.

“Mechi ilikuwa nzuri, Simba walikuwa kwenye ubora wao kipindi cha kwanza tulitimiza vizuri mipango yetu, lakini kwa kipindi cha pili wachezaji wangu walipoteza kujiamini nadhani Simba walipaswa kutupa adhabu kubwa zaidi ya hii walitugea, hongera kwao wamecheza vizuri,” amesema Mecky.

Katika hatua nyingine Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally jana alizindua hamasa Mbagara kuelekea mchezo wao wa Jumanne dhidi ya Wydad Casablanca.

Amesema mechi yao ya kuzi dhidi ya Kagera Sugar ilikuwa ina mambo mawili moja kutafuta ushindi na alama tatu na lingine ikiwemo mchezo huo kuwa sehemu ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Wydad Casablanca kumpelekea moto.

“Mechi ya leo (juzi) ni sehemua ya maandalizi ya mchezo wetu wa Jumanne, tumeona Benchikha alivyofanikiwa kuibadilisha timu, tulipoishia leo ndio itakuwa muendelezo dhidi ya Wydad Casablanca,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  WASIOOA WAKWAMWA KWA WALIOOA, WANYOOSHWA 3-0, ZACHAPWA KAVUKAVU