Habari za michezo
KISA KUSIMAMISHWA SIMBA….KAPAMA AVUNJA UKIMYA….AFUNGUA A-Z KINACHOENDELEA…
admin
December 21, 2023
7:46 pm
UONGOZI wa klabu umewasimamisha wachezaji wake wawili viungo, Clautos Chama na Nassor Kapama kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Taarifa kutoka idara ya Habari na Mawasiliano Simba inayosimamiwa na Ahmed Ally imesema hatua hiyo ni kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu kwa wachezaji hao watapelekwa katika Kamato ya nidhamu iliyopo chini ya Kamanda wa Polisi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, Seleman Kova.
Ilisema nyota hawa watapelekwa kwenye kamati hiyo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi za kimidhamu.
“Simba imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka kamati ya nidhamu wachezaji ili nao wao wapewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.
Uongozi unapenda kuwakumbusha watumishi wake kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu haitasita kumchukulia hatua yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo,” ilisema taarifa hiyo.
Alipotafutwa Kapama alisema taarifa hizo ameziona na ataenda katika kamati hiyo kusikiliza mashtaka yake.
“Kusema kweli sielewi, nimeona taarifa tu hivyo nitaenda kwenye kamati kusikiliza,” alisema nyota huyo.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.