Habari za Simba SC
Habari za michezo

AHMED ALLY AFUNGUKA SIMBA WATAKAVYOACHANA NA CHAMA….UTARATIBU WOTE HUU HAPA…

admin December 27, 2023 7:48 pm

Licha ya kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu, Uongozi wa Klabu hiyo umeweka bayana kuwa hakuna mpango wowote wa kutaka kumuachia, kutokana na mkataba wake ndani ya timu hiyo.

Kiungo huyo kutoka nchini Zambia na Uongozi wa Simba SC wamekuwa kwenye mvutano ambao umekuwa ukitajwa kama makosa ya utovu wa nidhamu wa mchezaji huyo ambao umepelekea kusimamishwa kwake.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa licha ya kiungo hiyo kusimamishwa lakini hawana mpango wowote wa kumuachia kutokana na kuendelea na progamu za benchi la ufundi.

Ahmed amesema kuwa mbali na kupewa adhabu ya kusimamishwa na kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu lakini kiungo huyo anaendelea na programu za mazoezi aliyopewa na benchi la ufundi pamoja na kulipwa stahiki zake ikiwemo mshahara wake.

“Chama amepata tuhuma za utovu wa nidhamu na amepelekwa katika kamati ya nidhamu, hatuna nia ya kuachana naye, hatuwezi kuachana na mchezaji ambaye bado ana mkataba na hatujapata hitimisho la adhabu yake ya utovu wa nidhamu.

“Kwetu ni mchezaji muhimu kama ilivyo kwa wachezaji wengine na hata ikifikia hatua ya kuamua kuachana naye basi ataondoka Simba SC kwa heshima zote,” amesema Ahmed.

UKWELI MCHUNGU…..KINACHOMTAFUNA MIQUISSONE SIMBA HIKI HAPA…. KUHUSU KUTUA YANGA….MSUVA KAIBUKA NA HILI JIPYA….AWATAJA SIMBA MAZIMA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “AHMED ALLY AFUNGUKA SIMBA WATAKAVYOACHANA NA CHAMA….UTARATIBU WOTE HUU HAPA…”

  1. manyama Timotheo says:

    Tunahitaji mabadiliko makubwa ndani ya kikosi cha timu yetu ya simba

Leave a Reply