Simba SC

Barker Aizidi Kete Yanga Kwa Makgalwa

Vardo July 10, 2026 3:17 pm

KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, anaonekana kuwazidi kete watani wao Yanga katika mbio za kumsajili winga wa Shekhukhune United ya Afrika Kusini, Keletso Makgalwa, kwa ajili ya msimu wa 2026/27.

Makgalwa ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakiwaniwa na vigogo hao wa soka la Tanzania, huku kila upande ukitajwa kuwasilisha ofa yake kwa lengo la kupata saini ya nyota huyo.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Makgalwa ameegemea zaidi kujiunga na Simba kutokana na ushawishi wa Barker, ambaye aliwahi kufanya kazi naye na anamfahamu vizuri uwezo wake.

“Simba wana nafasi kubwa ya kukamilisha usajili wa Makgalwa kutokana na ushawishi wa kocha Barker. Ingawa Yanga nao wameweka ofa mezani, inaonekana mchezaji ameonyesha kuvutiwa zaidi na mradi wa Simba,” amesema chanzo chetu.

Makgalwa amekuwa akiwindwa na klabu mbalimbali kufuatia kiwango chake kizuri akiwa na Shekhukhune United, jambo lililozifanya Simba na Yanga kuingia kwenye vita ya kuwania saini yake ili kuimarisha safu zao za ushambuliaji kuelekea msimu mpya.

Jux Anakula Tu Matunda Ya WCB Wasafi! Hakuna Pre-Season Ya Nje! Simba Yaweka Dau Kagame