Home Habari za michezo UWEPO WA MAXI KOMBE LA MAPINDUZI KOCHA ATOA TAMKO HILI

UWEPO WA MAXI KOMBE LA MAPINDUZI KOCHA ATOA TAMKO HILI

Habari za Yanga

Yanga imeanza maandalizi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 inayoanza Alhamisi, huku safu yake ya ushambuliaji ikizalisha mabao mengi ikiongozwa na Stephane Aziz KI aliyefunga 10, lakini kuna kocha mmoja amevunja ukimya na kutaka kiungo mshambuliaji, Maxi Nzengeli apumzishwe.

Maxi aliyesajiliwa msimu huu kutoka AS Maniema Union ya DR Congo, ametumika katika dakika 891 za mechi 11 za Ligi Kuu, huku akiwa amefunga mabao saba, lakini akishindwa kuwika kimataifa, Yanga ikicheza makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jambo hilo la kushindwa kuwika kimataifa, imemuibuka kocha wa zamani wa Yanga, Raoul Pierre Shungu, aliyesema anaiona kabisa timu hiyo ikienda robo fainali kutoka Kundi D, lakini akimtaka Miguel Gamondi kumpumzisha Maxi, ili awe moto zaidi.

Shungu aliyeiongoza Yanga hatua ya makundi kwa mara ya kwanza miaka 25 iliyopita kwa sasa anaiona AS Vita ya DR Congo, aliliambia Mwanaspoti kwa njia ya simu kuwa, kiungo huyo amekuwa akicheza michezo mingi bila kupumzika hali inayosababisha umakini wake kupungua.

Hivyo anatoa ushauri kwa benchio la ufundi la sasa la Yanga lililopo chini ya Gamondi, kuwa impe muda wa kupumzika ili awe mkali zaidi kwani kwa saa uchovu umemfanya apoteze nafasi nyingi uwanjani.

Kocha huyo alisema kucheza mara kwa mara kunasababisha mchezaji wakati mwingine kushuka kiwango kutokana na mwili kuchoka. “Maxi ni mchezaji anayejituma sana na umri mdogo alionao, nadhani tangu amefika Yanga amecheza mechi mfululizo kwa jinsi anavyopoteza nafasi nadhani anahitaji kupumzika kama kocha ataona inafaa,” alisema Shungu na kuongeza;

“Niliangalia ile mechi ya mwisho ya Yanga dhidi ya Medeama ya Ghana, nikaona jinsi umakini wake unavyopungua. Kuna wakati niliona wanachukua mpira hadi miguuni mwake, nadhani akipumzika atarudi na umakini lakini sijajua sasa ndani ya timu yao mechi zinapishanaje.”

Shungu alisema anaiona Yanga ikifuzu hatua ya robo fainali, kutokana na jinsi ilivyocheza mechi zote hususan ile ya mwisho dhidi ya Medeama.

“Kama wataendelea kucheza hivyo na kutumia nafasi, basi hakuna timu itakayowafunga tena katika mechi zilizosalia na itaenda hatua inayofuata.

“Yanga imekuwa ikicheza mpira mkubwa na ubora wake umeongezeka , inaweza kutinga robo fainali kama itaendeleza na kiwango ilikionyesha kwenye mechi ile basi itamaliza vizuri,” alisema Shungu.

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA WATULIZA VICHWA KIMATAIFA...... ISHU HII NDIO UMIZA KICHWA