Home Habari za michezo KUELEKEA AFCON ….WAZIRI WA MICHEZO ATAJA WACHEZAJI WAKUTUMIKA TAIFA STARS….

KUELEKEA AFCON ….WAZIRI WA MICHEZO ATAJA WACHEZAJI WAKUTUMIKA TAIFA STARS….

Taifa Stars

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro amewataka wadau wa Soka nchini kumuacha kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuwatumia wachezaji wanaocheza nje kama watafanya vibaya ndio aweze kulaumiwa.

Amesema kocha anatakiwa kufanya majukumu yake ya kuchangua wachezaji ambao anaimani wataipeperusha vema bendera ya Tanzania, kwenye michuano ya AFCON, yanayotarajiwa kufanyika, Ivory Coast, Januari 2024.

Taifa Stars iko kambini Visiwani Zanzibar kujiandaa na safari ya kwenda nchini Misri kati ya kesho au kesho kutwa na kuweka kambi hadi Januari 8, 2024 kwenda Ivory Coast tayari kwa michuano hiyo.

Waziri Ndumbaro amesema wakiangalia Tanzania ina wachezaji wengi katika mataifa mbalimbali ila wanaomba watanzania kumpa nafasi kocha Adel kufanya majukumu yake.

Amesema kocha bado hajaita kikosi cha cha wachezaji 30 ambao wataenda nchini Misri kwa ajili ya kambini na 25 watakaochaguliwa na Kocha Adel wataenda nchini Ivory Coast kwa ajili ya fainali ya AFCON.

“Ukiangalia Tanzania tumebarikiwa na wachezaji wengi na wote wazuri ila naomba watanzania kumpa nafasi Kocha kuitwa nyota watatufikisha katika malengo tunayatarajia kwa sababu anajua jukumu yale.

Tunatakiwa kumpa nafasi kufanya mipango yake na kusubiri matokeo mazuri na ndio tutachokidai kutoka kwake, ili timu ikishindwa ndio tumlaumu kocha kwa sababu ana uwezo wa kutueleza lolote,” amesema Ndumbaro.

Ameongeza kuwa baada ya kutangaza wachezaji hao kikosi kitaweka kambini Misri, timu inapokuwa huku itacheza mechi tatu za kirafiki, mchezo wa kwanza watacheza dhidi ua timu ya Taifa ya Misri.

Amesema mechi zingine mbili bado hawajaweka wazi watacheza na timu zipi kabla ya kwenda nchini Ivory Coast katika michuano hiyo ambayo mechi ya kwanza watacheza dhidi ya Morocco, Januari 17, mwakani.

“Tupo kundi F, Morocco, DR Congo, Zambia na sisi watanzania, sio kundi jepesi, tunaanza Morocco ukitaka kufanikiwa lazima umfunge bingwa, tunaenda Ivory Coast kupambana kupata matokeo mazuri.

Baada ya mchezo huo tutakuwa na Derby mbili ni ndugu zetu dhidi ya DR Congo ni Lake Tanganyika na mechi nyingine na Zambia ambao ni Tazara, Serikali, TFF na benchi la ufundi imejipanga vizuri kwa fainali hizi, Kocha Adel ametueleza kulingana na timu yake tunaenda kushindana,” amesema Waziri.

Amesema Serikali ina mchango mkubwa sana lakini niwaombe mashabiki nao waendelee kusapoti timu hamasa ya safari hii iwe ya juu hasa katika kila mechi za AFCON kuvaa jezi lakini kutumia mitandano ya kijamii kuizungumzia Stars.

“Mashabiki wana nafasi katika mchango wa timu tukumbuke Simba hivi karibuni walitwaa tuzo ya mashabiki bora hata Yanga wangepata sasa ile sifa yao ya kujaza uwanja wanatakiwa kuhamishia katika timu ya Taifa Stars,” amesema Waziri.

Ameeleza kuwa Wizara kushirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Januari 10, 2024 watafanya harambee kwa wadau mbalimbali na hizo fedha zitakazopatikq za timu mbili za Taifa Stars na Twiga Stars ambao nao wanaenda Morocco katika michuano ya WAFCON, 2024.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUMPA MSAMAHA...SIMBA WAAMUA 'KUJIMALIZA MAZIMA' KWA CHAMA....