Home Habari za michezo ALICHOSEMA BENCHIKHA BAADA YA KUWABUTUA KAGERA 3-0…ALIA NA UWANJA…

ALICHOSEMA BENCHIKHA BAADA YA KUWABUTUA KAGERA 3-0…ALIA NA UWANJA…

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amewasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Benchikha amesema uwanja haukuwa rafiki kiasi cha kuwanyima kucheza soka safi lakini hata hivyo amefurahi kwa ushindi huo mnono.

Aidha Benchikha amesema Kagera ni timu nzuri na waliwapa ushindani mkubwa pamoja na kuwa walikuwa bora na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Tumecheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu. Tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi

“Kagera ni timu nzuri wanacheza soka safi na walitupa ushindani mkubwa ingawa sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi,” amesema Benchikha.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAZIDI KUISHIKA CAF KILA KONA ....SIMBA MHHHH...