Home Habari za michezo BAADA YA KUWACHABANGA WAARABU LEO….RAIS SAMIA AFANYA KWELI SIMBA…..

BAADA YA KUWACHABANGA WAARABU LEO….RAIS SAMIA AFANYA KWELI SIMBA…..

Habari za Simba

Naibu Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mh. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amemkabidhi nahodha msaidizi wa Simba Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ milioni 10 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni zawadi ya ‘Bao la Mama’.

Rais Samia hutoa Shilingi milioni tano kwa kila bao litakalofungwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kuongeza morali kwa wachezaji.

Bao la mama limeongeza morali kwa wachezaji kujituma kuisaidia timu kupata matokeo ya ushindi.

Katika mchezo wa leo dhidi ya Wydad Casablanca mabao yote mawili waliyoshinda Simba yamefungwa na kiungo mshambuliaji, Willy Onana.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zikisomana lakini Wydad walifanya mashambulizi makali mawili dakika ya 28 na 32 lakini mlinda mlango wa Simba Ayoub Lakred alikuwa imara na kuondoa hatari zote.

Willy Onana aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 35 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kumalizia pasi ya kifua iliyopigwa na Kibu Denis.

Dakika mbili baadae Onana alifunga bao la pili baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Matokeo haya yameifanya Simba kufikisha pointi tano wakipanda hadi nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya vinara ASEC Mimosas.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Ngoma, Kibu (Duchu 67′), Mzamiru (Abdallah 79′), Beleke (Kennedy 79′), Chama (Bocco 60′), Onana (Israel 60′)

Walioonyeshwa kadi: Mzamiru 47′ Israel 80′ Lakred 89′ Abdallah 90+8.

X1: El Motie, Serrhat (Bahri 75′), Abdulfath, Haimoud, El Idriss, Harkass, Draoui, Lahtimi (Ounnajem 45′),Amloud, (Moutaraji 45′) Sambou, Bouhra

SOMA NA HII  HII HAPA NDIO MITEGO MIWILI YA YANGA