Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAGHANA….GAMONDI ATAJA MABADILIKO HAYA YANGA…MASTAA KUKOSEKANA..

KUELEKEA MECHI NA WAGHANA….GAMONDI ATAJA MABADILIKO HAYA YANGA…MASTAA KUKOSEKANA..

Habari za Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi atafanya mabadiliko madogo ya kikosi chake kuelekea mechi yao ya mkondo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama FC.

Mabadiliko hayo yatakuwa katika safu ya ulinzi baada ya beki Joyce Lomalisa kutokuwepo kwenye mipango ya mchezo huo baada ya kuumia kwenye mchezo wa Al Ahly ya Misri na nafasi yake kuchukuliwa na Nickson Kibabage.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Gamindi kimeondoka jana usiku kuelekea Ghana kwa ajili ya kusaka alama tatu muhimu huku Lomalisa hatokuwepo sehemu ya mchezo huo kutoka na kupata jeraha kwenye mechi iliyopita na yuko katika uchunguzi wa kujua kiasi gani ameumia.

Yanga imefanikuwa kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 imekusanya alama moja na inapeperusha bendera ya Tanzania katika michuano hiyo ina kibarua kiguma Ijumaa hii, uwanja wa Baba Yara, uliopo mji wa Kumasi nchini humo.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema wachezaji wote wako na morali kubwa kwenda kutafuta furaha za mashabiki wa Yanga na kufikia malengo yao.

Amesema katika kikosi hicho hatakuwepo Lomalisa ambaye yuko kwenye uchunguzi baada ya kuumia katika mechi iliyopita dhidi ya Al Ahly na nafasi yake kuchukuliwa na Kibabage .

“Ni kweli tutamkosa Lomalisa lakini hatuna presha kutokuwepo kwake kwa sababu yupo Kibabage ni mzuri na kufanya kazi yake ipasavyo tumeshamuona katika michezo junsi alivyokuwa akicheza.

Presha ya mchezo lazima kwa sababu kila dakila 90 zinapokamilika basi mahesabu yanabadilika , mchezo ni mgumu tunaenda kucheza ugenini na ukizingatia Medeama wamemfunga alitetufunga CR Belouizdad hivyo watakuwa na kujiamini.

Watambue tu kuwa Yanga sio mpinzani mwepesi tunahitaji kutafuta matokeo mazuri ikiwemo ni ushindi ili hesabu zetu ziweze kukamilika,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa wanatambua katika historia walipoteza ugenini 3-1 mwaka 2016 na katika mcheso wa marudiano kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani, wanasahau hayo na wanaenda kutafuta ushindi ili kukamilisha hesabu zao.

“Tunajua historia lakini hesabu zetu ni jinsi ya kufikia malengo yetu, tumepoteza mechi mmoja, kutoka sare mmoja sasa tunahitaji alama tatu za michezo iliyopo mbele yetu tukianza dhidi ya Medeama ,” amesema Meneja huyo wa habari.

SOMA NA HII  RASMI..ISHU YA DODOMA JIJI NA DJUMA YAFIKIA MWISHO..UONGOZI WAIBUKA NA KUTOA TAARIFA HII...