Klabu ya Young Africans imesema imebakiza nafasi mbili za Usajili, ikiweka wazi aina ya wachezaji itakaowasajili kuwa ni wale tu ambao hawajacheza mechi zozote za Kimataifa wakiwa na timu zao msimu huu.
Makamu wa rais wa klabu hiyo, Arafat Haji, amesema kuwa, zipo tetesi nyingi zikiihusisha Young Africans kusajili wachezaji mbalimbali wakiwamo wa timu za Medeama ya Ghana, Jwaneng Galaxy ya Botswana na Asec Mimosas ya Ivory Coast, lakini Ukweli ni kwamba watasajili wachezaji ambao timu zao hazikucheza michuano hiyo ili wakishasajiliwa wasibanwe kucheza michuano hiyo.
“Tunataka wachezaji ambao tukiwasajili waingie moja kwa moja kuisaidia timu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, Wachezaji wa timu hizo hata kama tukiwasajili hawatocheza kwa hiyo hakuna faida yoyote.
“Malengo yetu kwenye kikosi ni kupata wachezaji ambao wataingia moja kwa moja kwenye kikosi na kucheza michuano ya kimataifa, kwa hiyo yeyote ambaye atasajiliwa basi ni yule ambaye hajacheza kabisa michuano hiyo.
“Nani anaingia watu wameanza kuona, tumeanza kwa kumsajili Shekhan lbrahimn Khamis na wa pili ni Augustine Okrah, lakini nani anatoka bado tutakuja baadae kuwaeleza Wanayanga,” amesema Arafat.
Amesema kwa sasa wanaendelea kuifanyia kazi ripoti ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, ambaye amewaambia kuwe na maingizo ya wachezaji wachache, hasa kwenye dirisha dogo ambalo lina uhaba wa wachezaji wengi bora walio huru.
“Kipindi hiki cha dirisha dogo ni mara chache sana kuweza kufanikis