Habari za Simba leo
Habari za michezo

SIMBA WAPELEKA JEZI IKULU ZNZ….

admin January 5, 2024 7:21 am

Makamu wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abbullah ameupogeza uongozi wa Klabu ya Simba kwa kuamua kutangaza Utalii wa Zanzibar kupitia michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mh. Abdullah amesema Simba imefanya jambo zuri kutangaza Utalii kwakuwa ni timu kubwa na ina wafuasi wengi hivyo tunafika sehemu kubwa duniani.

“Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar naupongeza Uongozi wa Simba kwa kuamua kutangaza Utalii wetu, hili ni jambo kubwa mmefanya na mnastahili pongezi,”amesema Mh. Abdullah.

Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amemueleza Mh. Abdullah kuwa mipango ya Simba ni kutumia michuano ya Mapinduzi kusaidia kukuza uchumi kupitia kutangaza Utalii.

“Simba ni Klabu kubwa na tuna wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii tumeona kupitia michuano hii itakuwa fursa kwetu kuutangaza Utalii na tunafahamu ndio chanzo kikuu cha pato la taifa hili,” amesema Ahmed.

SIMBA YASHUSHA JEMBE USIKU MNENE….OKRAH ABEBWA NA HAYA YANGA… MASHINE MPYA YA SIMBA HII HAPA….JAMAA NI KIFAA NA NUSU….BENCHIKHA APITISHA TIKI NYEKUNDU..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply