Habari za Yanga leo
Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUFUNGWA JANA….ALLY KAMWE KAIBUKA NA HILI JIPYA LA KUTULIZIA HALI….

admin January 8, 2024 11:18 am

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa yote yalitokea katika Kombe la Mapinduzi 2024 wanashukuru huku safari yao ikigotea robo fainali.

Chini ya Miguel Gamondi katika mechi tatu za hatua ya makundi ndani ya dakika 270 ilishinda mbili na kuambulia sare moja ikakomba pointi 7 kati ya 9.

Januari 7 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Amaan ukisoma Yanga 1-3 APR FC ukiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali na wa Kwanza kwa Yanga kupoteza.

NI Jesus Moloko alifungua pazia la mabao dakika ya 23 likawekwa usawa na Soulei Sanda dakika ya 45 kisha kipindi cha pili APR waoiongeza mabao mawili kupitia kwa Mbaoma Victor dakika ya 49 kwa mkwaju wa penalti na Sharaf Eldin Shaiboub dakika ya 79 alifunga bao la tatu.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema:” Kwa kilichotokea tunamshukuru Mungu kwa kuwa safari yetu umeishia hatua ya robo fainali katika Mapinduzi 2024 hivyo tunajipanga kwa wakati ujao,”.

Watani zao wa jadi Simba wanatarajiwa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali watakutana na Jamhuri kwenye hatua ya robo fainali, Januari 8.

YANGA WAFUATA STRAIKA ULAYA…SIMBA YAGOMA KURUDIA MAKOSA…SARR ACHANA MKATABA… KIPIGO KUTOKA MISRI JANA CHAMFANYA SAMATTA KUJA NA KAULI HII YA KISHUJAA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply