Home Habari za michezo AISHI MANULA AUNGANA NA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUZINDUA SPARK 20...

AISHI MANULA AUNGANA NA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUZINDUA SPARK 20 SERIES…

Tecno

Kampuni ya simu za mkononi TECNO Mobile Tanzania iliungana na wanafunzi wavyuo katika uzinduzi wa simu mpya ya TECNO SPARK 20 Pro+, SPARK 20 Pro na SPARK 20 uliofanyika katika ukumbi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ‘UDSM’.

Uzinduzi wa TECNO SPARK 20 Series uliambata na utambulisho wa kampeni yenye kumlenga mtoto mwenye kipaji cha mpira iliyopewa jina la BUSTI KIPAJI.

katika kufikisha taarifa yake balozi matoleo ya SPARK 20 Bwana Aishi manura kijana anayekipiga katika timu ya Taifa Tanzania na Club ya Simba alifikisha taarifa yake kwa watanzania kuchangia kumsaidia mtoto wa Kitanzania katika kufikia malengo yake kupitia kipaji.

“hapo awali nikiwa mdogo sikuwa na viatu vya kuchezea mpira hivyo nilikuwa nikipata majeraha kutokana na kuwa wale wenzangu niliokuwa nikicheza nao wazazi wao waliweza wapatia viatu sahihi kwajili ya mchezo wa mpira wa miguu, sasa basi wa yeyote atakayenunua toleo lolote la SPARK 20 moja kwa moja atakuwa amemvisha kiatu kijana huyo kwa sababu kwa asilimia ya pesa utakayolipia kwajili ya SPARK kiasi kadhaa kitaenda kumvisha kiatu kijana huyu kama kampeni yetu inavyosema BUSTI KIPAJI”.

Tecno Spark 20 ProMeneja Masoko TECNO Tanzania Salma Shafii pia alipata wasaa wakuilezea TECNO SPARK 20 Pro + kwa ufupi, ni simu nzuri yenye teknolojia ya kisasa kuanzia muundo ni wa kisasa kwa lugha ya rahisi tunasema 3D curved yani imepinda pembezoni mwa kioo, ina processor yenye speed nzuri nayo ni Mediatek Helio G99 na camera ya kisasa yenye Megapixel 108 iliyoongezewa teknolojia ya 9 n’ 1 ili kuongeza mwanga zaidi katika uchukuaji picha na kuifanya picha ing’ae zaidi hasa katika nyakati za usiku.  Spark 20 series pamoja ya kuwa na sifa ambazo zitamnufaisha mwanafunzi wakati wa kujisomea, kuangalia mpira au kazi nyengine yoyote lakini pia tumeweka unafuu kwenye bei”.

Meneja Masoko TECNO Tanzania Salma Shafii.

SPARK 20 Pro+ ipo madukani kwa bei ya shilling 672,600, SPARK 20 Pro 578,200 na shilling 365,800 SPARK 20”. SPARK 20 Series inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania kwa bei tajwa hapo juu kwa maelezo zaidi watembelee @tecnomobiletanzania. #Spark20CampusLaunch

SOMA NA HII  BAADA YA KUMLAZA MAYELE KWENYE UFUNGAJI BORA...GEORGE MPOLE AIBUKA NA HILI JIPYA...ATAJA KLABU ATAKAYOICHEZEA...