WINGA mpya wa Simba, Ladack Chasambi amesema anatambua kuwa amejiunga na timu yenye wachezaji wakubwa na anatarajia kupata ushindani mkubwa wa kuwania namba, lakini atahakikisha anajituma mazoezini kwa ajili ya kumshawishi Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha ili awemo kwenye kikosi chake cha kwanza.
Chasambi amesaini mkataba wa miaka mitatu na amejiunga na kikosi cha Simba kilichopo Visiwani Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo Wekundu hao wa Msimbazi wametinga hatua ya nusu fainali.
Inafahamika kuwa Chasambi atakuwa akilipwa mshahara wa Milioni 3.5 kwa mwezi, sambamba na kupewa gari kwa ajili ya matumizi yake, aidha ikitokea klabu itataka kumnunua , mkataba wake umebainisha kuwa atauzwa kwa dola 600,000 sawa na Bilioni 2 na zaidi.
Chasambi amesema amefurahi kujiunga na klabu kubwa ya Simba ambapo mara nyingi kunakuwa na changamoto kwa wachezaji wengi wa kizawa wanapokwenda kwenye klabu hizo kubwa, lakini kwake anajiamini na ambacho kitampa nafasi ni kujituma na bidii ya mazoezi.
Amesema katika nafasi yake kuna wachezaji wengi wenye uwezo ndani ya Simba lakini anaimani kujiunga ndani ya kikosi hicho ni sahihi kupata viri vya kujifunza kutoka kwa wakubwa wake ambao wako kwenye kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.
“Sina hofu juu ya ushindani wa namba uliopo ndani ya Simba, kikubwa natakiwa kujituma kwenye mazoezi na hata mechi nikipewa nafasi ya kucheza ili kuendelea kumshawishi kocha kunipa nafasi ndani ya kikosi chake cha kwanza.
Ni ngumu kuingia kwenye timu na kupata nafasi moja kwa moja natakiwa kupambana, kujituma na kushirikiana na wachezaji wenzangu katika mechi na kufanikiwa tunafikia malengo yanayotarajiwa,” amesema Chasambi.
Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema usajili wa winga Chasambi utakuwa na manufaa makubwa kutokana na ubora na umri alionao.
Amesema Chasambi ni mchezaji kijana mwenye kipaji kikubwa kulingana kile alichokionyesha kwenye timu aliyotoka, baada ya kutua Simba, anaingia kwenye kikosi rataribu ili aside na presha
“Hatutaki kumpa presha mchezaji wetu kijana, kocha Benchikha ameridhika na usajili wa dogo na tunamuacha afanye kazi yake uwanjani kuonyesha kile tunachokitarajia kutoka kwake akishirikiana na wachezaji wenzake,” amesema Ahmed.
Kagere ame zinguwa