Kikosi cha Simba kimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Singida Fountain Gate kwa mikwaju ya penati 3-2 kufuatia kutoka sare kwenye muda wa kawaida.
Elvis Rupia aliwapatia Singida bao la mapema dakika ya 11 baada ya mlinzi wa Simba Kennedy Juma kukosea kuokoa na kumpa mpira Marouf Tchakei ambaye alitoa pasi kwa mfungaji.
Kipindi cha pili Simba iliongeza kasi ya kutafuta bao la kusawazisha lakini Singida walikuwa makini katika safu ya ulinzi kuhakikisha wanakuwa salama muda wote.
Fabrice Ngoma aliipatia Simba goli la kusawazisha dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya mpira na kona uliopigwa na Saido Ntibazonkiza kuokolewa kabla ya kumkuta mfungaji akiwa ndani ya 18.
Kwa matokea haya, Simba itacheza na Mlandege kwenye mchezo wa Fainali utakaopigwa tarehe 13 mwezi huu kwenye uwanja wa New Aman Complex.
Mshindi kwenye mchezo huo anatazamiwa kupata Kombe pamoja na zawadi ya Milioni 100, huku mshindi wa pili akiambulia Milioni 50.
Vikosi vilivyoanza leo kwa timu zote mbili ni pamoja na