Home Habari za michezo HUU HAPA MPIRA RASMI WA AFCON NA RATIBA YA MECHI ZA TAIFA...

HUU HAPA MPIRA RASMI WA AFCON NA RATIBA YA MECHI ZA TAIFA STARS…

Habari za Michezo leo

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limezindua na kutambulisha mpira rasmi utakaotumika kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 zitakazofanyika nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 huku ukipewa jina la gwiji wa taifa hilo, Pokou.

Mpira huo umepewa jina Pokou ikiwa ni heshima kwa staa wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Pokou, ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora mara mbili wa michuano ya Afcon 1968 na Afcon 1970 huko Sudan alikofunga mabao sita na manane mtawalia.

Katika fainali ambazo Pokou alimaliza kwa mabao manane, matano alifunga kwenye mechi moja, wakati kikosi cha Tembo kilipoichapa Ethiopita 6-1.

Novemba 13, 2016, Pokou alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 69 akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora kwenye Afcon mara mbili, akipachuka jumla ya mabao 14, manne nyuma ya kinara wa muda wote wa mabao kwenye fainali hizo za ubingwa wa Afrika, Mcamerooni, Samuel Eto’o mwenye mabao 18.

Mpira wa Pokou, ambao utatumika kwenye fainali hizo za 34 za ubingwa wa Afrika, umetengenezwa kwa rangi mchanganyiko ikiwamo nyeupe, kijani, machungwa ikiwakilisha bendera ya taifa la Ivory Coast.

Mbali na mpira huo kupewa jina la Fokou, kuna kuna uwanja mmoja pia utatumia jina hilo, ambao utashuhudia mechi ya Kundi FA baina ya Taifa Stars dhidi ya Morocco, Januari 17 na dhidi ya Zambia, Januari Januari 21. Mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, Stars itakipiga na DR Congo, Januari 24 kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Karhogo.

SOMA NA HII  SIMBA BAADA YA KUMPA THANK YOU SAWADOGO, MAPYA YAIBUKA