Home Habari za michezo PANGA LA YANGA KUPITA NA MASTAA HAWA….ENG HERSI ATAJA MAJINA….

PANGA LA YANGA KUPITA NA MASTAA HAWA….ENG HERSI ATAJA MAJINA….

Habari za Yanga leo

RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema wachezaji ambao hawana mchango wowote kwenye kikosi hawana nafasi ndani ya timu hiyo.

“Katika usajili tunaofanya matarajio yetu ni kuona mchezaji anatupa matokeo uwanjani, kama hawezi uwanjani hakuna sehemu nyingine atatuonyesha uwezo, hivyo hakuna nafasi kwake,” amesema.

Kiongozi huyo wa Yanga amesema hakutakuwa na presha kwa viongozi au benchi la ufundi kwa mchezaji ambaye ameshindwa kutimiza majukumu yake uwanjani kwa sababu hafai kuwa mchezaji wa timu hiyo.

“Katika wachezaji waliopo Yanga sasa hivi kwa asilimia 90 wote nimehusika kwenye usajili wao Diarra, Mshery, Kibwana, Kibabage, Lomalisa, Job, Mwanyeto, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki,” amesema.

“Mimi ni rahisi wa klabu ya Yanga hivyo wote ni wachezaji wangu kwasababu wanavaa jezi ya klabu ninayoiongoza,” alisema Hersi kwenye moja ya mahojiano na kituo cha Clouds Media.

Kwa mujibu wa kauli ya Rais wa Yanga, mastaa ambao wanatakiwa kupisha usajili mpya dirisha hili la usajili kutokana na namba ni pamoja na Crispin Ngushi ambaye amecheza dakika 11 msimu huu kwenye mechi 10 za ligi walizocheza.

Hafiz Konkoni amecheza dakika 189 na ndiye mchezaji ambaye alisajiliwa kwa matarajio makubwa ili kuziba pengo la Fiston Mayele eneo la ushambuliaji ambalo sasa wanapambana kusaka mshindani.

Fred Gift ni beki wa kati wa timu hiyo ambaye tangu amesajiliwa licha ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara amecheza dakika 21 tu na ameshindwa kutoa changamoto kwa wazawa wanaomuweka benchi.

Jonas Mkude amesajiliwa msimu huu akitokea Simba tangu ametua kikosini humo amecheza dakika 14 kwenye mechi mbili ambazo kila moja amecheza dakika saba.

Denis Nkane amecheza dakika 40 na anatajwa kutakiwa kujiunga na Dodoma Jiji kwa mkopo kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango chini ya kocha Miguel Gamondi.

Licha ya kutumika kwa dakika nyingi kidogo winga Ducapel Moloko anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaopisha usajili mpya kutokana na kushindwa kufanya kile alichokifanya msimu uliopita amecheza dakika 334.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUFUKUZWA ...ADEL ZRANE AIBUKA NA KUFICHUA YA SIMBA...AGUSIA USAJILI ...