Home Habari za michezo WAKATI MICHANGO IKIENDELA BONGO….KOCHA TAIFA STARS ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI..

WAKATI MICHANGO IKIENDELA BONGO….KOCHA TAIFA STARS ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI..

Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Stars, Adel Amrouche amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kucheza kwa bidii na kuonyesha vipaji vyao katika mechi ya kwanza ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco utakaochezwa kwenye uwanja wa San Pedro nchini Ivory Coast, Januari 17.

Mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, mwaka huu Tanzania ikimenyana na Morocco, DR Congo na Zambia katika kundi F.

Kocha Amrouche amesema amefanyia kazi mapungufu ya kikosi chake katika mechi iliyopita ya kirafiki na Misri na kuwataka wachezaji kupambana katika mchezo iliyopo mbele yao.

Amesema bado hajashtushwa na matarajio ya kukabiliana na wapinzani wakubwa, wanaelewa changamoto iliyo mbele yao kwa kusahihisha makosa yao kabla ya kuvaana na Morocco.

“Hii ni fursa kubwa kwa wachezaji kuyatumia mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya kuonyesha uwezo mzuri lakini lengo letu la msingi ni kutoa matokeo bora na kuacha kila kitu uwanjani.

Mashindano hayo yanatoa nafasi ya kujipima dhidi ya bora zaidi barani Afrika, nina matumaini makubwa ya kufanya vizuri kulingana maandalizi ya timu tuliyofanya, wachezaji wakitenda vizuri na kuhamisha ya mazoezi na kupeleka uwanjani watafanya vizuri zaidi katika makundi,” amesema Amrouche.

Naye Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema, wamekuwa wakishiriki tu mashindano hayo, sasa hivi wamejipanga kuhakikisha wanafuzu hatua inayofuata.

“Tumejiandaa vizuri, tunaamini kwa kushirikiana kwa pamoja tutafikia malengo yetu, mara hii hatutaki kuishia hatua ya makundi angalau tufike hata robo fainali.Tunataka kuweka rekodi mpya, tumechoka kuishia hatua ya makundi ya michuano hii, kila mchezaji anatamani kufanya vizuri, kwa msaada wa Mungu na maombi ya Watanzania naamini tutafikia malengo yetu,” amesema Samatta.

Ameongeza kuwa wanatambua wanakutana na timu nzuri katika kundi lao na wanaiheshimu kila timu wanayokutana nayo katika hatua ya makundi ili kusonga mbele.

“Ukiliangalia kundi tulilopo sio jepesi, tunatakiwa kuwaheshimu wapinzani wetu kinachotakiwa ni kujiandaa kwa ajili ya kushindana na sio kushiriki,” amesema.

SOMA NA HII  AVITOR BETI ZA BURE SIKU 30 MWEZI NOVEMBA