Habari za Simba leo
Habari za michezo

SHOW ZA NGOMA ZAMFANYA BENCHIKHA KUIBUKA NA HILI…AWAPA MAAGIZO MABOSI SIMBA..

admin January 15, 2024 6:42 am

KOCHA Mkuu wa Simba, Mualgeria Abdelhak Benchikha amefunguka kukoshwa na kiwango cha nyota wake, Fabrice Ngoma huku akisema kuwa amekuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo jambo ambalo kwake kama mwalimu anavutiwa nalo.

Ngoma ambaye amesajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Al Hilal ya Sudan, ni moja kati ya wachezaji wenye uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana uwezo mkubwa anaouonyesha katika eneo la kiungo cha timu hiyo.

Kocha Benchikha alisema kuwa: “Ngoma ndio ni moja kati ya wachezaji ambao wameonekana kuwa na umuhimu katika kikosi changu lakini hilo sio kwangu pekee bali kote ambapo amepita Ngoma alikuwa anafanya vyema.

“Ni mchezaji ambaye huwa anapenda kuutawala mchezo lakini mara nyingi amekuwa akionyesha ile kiu ya kutaka kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri na inapata matokeo,hii imekuwa faida kwetu kwa Simba.

“Tunataka kuona timu kama Simba inakuwa na wachezaji wengi wenye uwezo na kuisadia timu kuzidi kuwa kubwa na yenye uwezo wa kuyapata mafanikio na hapo itakuwa ni faida zaidi kwetu katika mipango yetu ambayo tumejiwekea,” alisema Benchikha.

BENCHIKHA AWA MBOGO SIMBA….GAMONDI AJIPA SIKU 38 YANGA…. KUMBE ALIYEWATIA UCHUNGU SIMBA JUZI NI ‘MCHEZAJI WA NDONDO’…HANA MKATABA NA MLANDEGE..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply