Habari za Yanga leo
Habari za michezo

SIKU CHACHE TOKA ‘AFYEKWE’ YANGA….MOLOKO AENDEELA KUFUNGUKA YA MOYONI…AJA NA HILI…

admin January 19, 2024 6:14 am

Aliyekua Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ wa Young Africans, Jesus Moloko, amesema anaondoka Tanzania huku akiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindani uliopo katika Ligi Kuu Bara.

Rasmi Young Africans mwanzoni mwa juma hili ilitangaza kuachana na winga huyo kwa makubaliano ya pande zote, baada ya kudumu katika kikosi chao kwa muda wa miaka mitatu.

Moloko, amesema hataisahau Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na ushindani wake, lakini pia mapenzi ya mashabiki kwa klabu zao na wachezaji.

“Nimeishi vizuri sana hapa Tanzania, sitaisahau ligi ya hapa, imekuwa na ushindani, na kikubwa namna mashabiki wanavyopenda vilabu na wachezaji wao, hili ni jambo la kujivunia sana kwa watanzania,” amesema Moloko.

Ameongeza kuwa anarudi nchini kwao kuanza maisha mapya ya soka na kila kitu kitajulikana baada ya kufika huko, kwa sababu bado ana uwezo wa kucheza soka kwa kiwango cha juu.

“Nitaendelea na maisha ya soka, kwa sasa narudi Congo (DRC), kujipanga, na najua nitapata timu muda ukifika, bado nitaendelea kucheza soka,” Moloko ameongeza.

Winga huyo pia ameushukuru uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompatia katika muda wote akiwa ndani ya timu hiyo.

BAADA YA KUONA MZIKI WA SIMBA ULIVYO….SARR AENDA KWAO SENEGALI ‘KUJIBUSTI’…. MAKOCHA WAPISHANA KAULI ISHU YA BALEKE NA PHIRI KUACHWA PAMOJA SIMBA…ISHU HII HAPA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “SIKU CHACHE TOKA ‘AFYEKWE’ YANGA….MOLOKO AENDEELA KUFUNGUKA YA MOYONI…AJA NA HILI…”

  1. William Lema says:

    Ukijiheshimu unaheshimiwa

Leave a Reply