Habari za Michezo leo
Habari za michezo

DILI LA MSUVA NA YANGA ZIIIIII….MATAJIRI WA AFRIKA KUSINI WAMBEBA JUU KWA JUU…

admin January 20, 2024 10:08 pm

SIMON Msuva winga mzawa ambaye yupo na timu ya Tanzania, Taifa Stars, Ivory Coast kwenye Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) amesaini dili la miaka miwili Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini.

Nyota huyo aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Yanga ambapo alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za kurejeshwa hapo kwa mara nyingine tena.

Taarifa zimeeleza kuwa mchezaji huyo amesaini dili la mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo hivyo hatajiunga na Yanga wakati huu mpaka wakati ujao ikiwa watafikia makubaliano mazuri.

Timu ya Taifa ya Tanzania inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili hatua ya makundi wakiwa kundi F itakuwa dhidi ya Zambia.

Januari 21 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa baada ya ule wa awali Januari 17 kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco ambapo Msuva anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa kwenye kazi hiyo.

Kwa sasa alikuwa mchezaji huru baada ya kutokuwa na timu kwa kuwa ile aliyokuwa awali ilisitisha mkataba wake.

MABOSI SIMBA NI NOMAA….WAWAPA MASTAA WAPYA MIKATABA YA KIMAFIA MWANZO MWISHO… HIZI HAPA SABABU ZA KIGOGO WA SERIKALI KUIKIMBIA SINGIDA FG..,FIFA WATAJWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply