Home Habari za michezo PAMOJA NA KUMFUNGIA AMROUCHE…, CAF WASHUSHA RUNGU LA PILI KWA TANZANIA….

PAMOJA NA KUMFUNGIA AMROUCHE…, CAF WASHUSHA RUNGU LA PILI KWA TANZANIA….

Habari za Michezo leo

Shirikisho la Soka Afrika CAF limetoa taarifa rasmi juu ya kumfungia kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche na kuitoza faini Tanzania (TFF) dola za kimarekani 10,000 (Ths 27,000,000/=)

CAF katika taarifa yao wanasema Amrouche amekutwa na hatia kwa kukiuka vifungu vya kanuni za nidhamu namba 82, 83, 84 na 131.

Amrouche ambaye ameonyesha nia ya kukata rufaa bado yupo na Stars huko Ivory Coast ingawa tayari TFF wamemsimamisha kazi na majukumu yake wamepewa wazawa Hemedi Morocco na Juma Mgunda.

Tanzania iko nchini Ivory Coast kwenye michuano ya 34 ya AFCON, ambapo tayari imeshacheza mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo ilifungwa magoli 3-0.

Leo hii Taifa Stars itashuka tena uwanjani kupepeptana na Zambia katika mechi ya pili na muhimu kwani ushindi utaifanya Tanzania kuanza kukusanya pointi katika kundi lake.

Hata hivyo, Tanzania leo itakuwa chini ya Makocha wazawa Hemed Morocco akisaidiana na Juma Mgunda ambao wamekasimishwa madaraka hayo na TFF.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI