Habari za Michezo leo
Habari za michezo

KISA CHILUNDA…KMC WAANZA KUWAZIA YA CAF MAPEMA….

admin January 30, 2024 10:31 am

Uongozi wa KMC FC umetamba na usajili wachezaji wao wapya akiwemo Shaban Chilunda kuwa utawafanya kuwa imara zaidi huku wakiweka malengo yao ya kutaka kumaliza ligi wakiwa ndani ya nne bora ili waweze kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Chilunda ni moja ya nyota wapya wa KMC ambaye amesajiliwa katika dirisha dogo akitokea Simba SC ambapo pia yupo beki, Abdalla Said Lanso kutoka visiwani Zanzibar:

Ofisa Habari wa KMC, Khalid Chukuchuku ametamba kwa kusema kuwa: β€œUsajili ambao KMC tumeufanya katika dirisha dogo utaona ni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu kwa ajili ya kuendelea kufanya vyema.

Tungeweza kufanya usajili hata wa wachezaji wanne au watano ambao tungewajaza bila sababu, lakini sisi tumefanya usajili wa maana na wenye tija na malengo yetu ni kuhakikisha kuwa tufanya vizuri ili tumalize ligi nafasi za nne za juu.

β€œMalengo yetu ni kushiriki michuano ya kimataifa na kwa usajili huu naamini utatusaidia kutimiza malengo yetu kwa ajili ya msimu ujao,” amesema kiongozi huyo.

CHAMA NA SIMBA SASA MAMBO NI BAMBAM….BENCHIKHA MENO YOTE NNJE…. PACOME APELEKEWA AL AHLY….GAMONDI AANZA KUFANYA YAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “KISA CHILUNDA…KMC WAANZA KUWAZIA YA CAF MAPEMA….”

  1. BENSON says:

    Mchezaji mzuri

Leave a Reply