Habari za Simba leo
Habari za michezo

CHAMA NA SIMBA SASA MAMBO NI BAMBAM….BENCHIKHA MENO YOTE NNJE….

admin January 30, 2024 10:26 am

Kiungo Clatous Chama amesamehewa na Uongozi wa Simba SC na Februari 01 atajiunga na wenzie kambini kwa ajili ya michezo ya mzunguuko wa pili wa ligi pamoja na maandalizi ya mchezo wa CAFCL dhidi ya Asec Mimosas, mchezo utakaochezwa nchini Ivory Coast.

Clatous Chama atakuwepo michezo miwili ya ugenini ya viporo Simba SC dhidi ya Mashujaa FC na Tabora United, mchezo wa Januari 31 hatakuwa sehemu ya mchezo

Itakumbukwa kuwa Chama, alisimamishwa pamoja na Nasorro Kapama katika kile kilichosemekana kuwa walifanya makosa ya kinidhamu.

Hata hivyo, Kapama yeye aliomba kuondoka kwenye klabu hiyo kwenye dirisha dogo la mwezi huu mara baada ya kutopata nafasi ya kucheza.

Kusamehewa kwa Chama kutamfanya Kocha MKuu wa Simba , Benchikha kuwa na uhakika wa kikosi chake kutengeneza magoli mengi zaidi, haswa mara baada ya kusajili washambuliaji wapya.

Simba itashuka dimbani kesho kutwa kwenye mchezo wa hatua ya 16 ya Michuano ya ASFC dhidi ya Tembo katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex .

WAKATI TFF WAKIUMA MENO….ZFF WATIA ‘UBANI’ OMBI LA SIMBA KUTUMIA UWANJA WA AMANI.. KISA CHILUNDA…KMC WAANZA KUWAZIA YA CAF MAPEMA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

3 responses to “CHAMA NA SIMBA SASA MAMBO NI BAMBAM….BENCHIKHA MENO YOTE NNJE….”

  1. Mophety says:

    Endleen kupga kazi,,lakin habari na taarifa zenu ziwe za kweli na uhakika

  2. Mophety says:

    Good news

  3. Edgar says:

    🙏🙏🤝👏

Leave a Reply