Home Habari za michezo JEMBE LA BENCHIKHA NDANI YA SIMBA LATAJA SIKU YA KURUDI RASMI KUKIWASHA…..

JEMBE LA BENCHIKHA NDANI YA SIMBA LATAJA SIKU YA KURUDI RASMI KUKIWASHA…..

Habari za Simba leo

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Muivory Coast, Aubin Kramo ametaja siku atakayorejea kuichezea timu hiyo, huku akiahidi kuifanyia makubwa.

Kiungo huyo yupo nje ya uwanja muda akiuguza majeraha ya goti ambayo alifanyiwa operesheni. Nyota huyo alifanyiwa operesheni hiyo nchini Afrika Kusini baada ya Madaktari kushauri.

Kramo alisema kuwa rasmi anatarajiwa kurejea uwanjani mapema Machi, mwaka huu baada ya kupona kamili.

Alisema kuwa baada ya kurejea uwanjani atahakikisha anafunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Bara au Ligi ya Mabingwa Afrika kama shukrani kwa mashabiki kumvumilia.

“Nawapenda mashabiki wa Simba ambao wamekuwa wavumilivu na kunifariji kwa kipindi chote nilichokaa nje ya uwanja.

“Hivyo nimewaandalia zawadi kwao kwa kufunga bao baada ya kurejea mwezi Machi, mwaka huu baada ya kupona,” alisema Kramo.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO DILI LA MAKUSU YANGA LILIPOFIKIA...FRAGA KUKABIDHIWA MIKOBA YA LWANGA SIMBA...