Home Habari za michezo AHMED ALLY: AL AHLY, MAMELOD, ZAMALEKH NA MAZEMBE WANASUBIRI KWA HAMU KUJUA...

AHMED ALLY: AL AHLY, MAMELOD, ZAMALEKH NA MAZEMBE WANASUBIRI KWA HAMU KUJUA USAJILI WETU MSIMU HUU…


Ahmed Ally; ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba ambaye anasema muda si mrefu timu hiyo itaanza kushusha wachezaji wapya ambao tayari imewasajili.

Ahmed Ally anasema; “Tumeshamaliza kukisuka kikosi chetu. Wote tuliowahitaji wapo kwenye makaratasi yetu, muda si muda tutaanza kushusha vyuma.

“Al Ahly, Raja, Mamelod, Mazembe, Zamalekh, Wydad wanasubiri kwa hamu kuona tumesajili nani maana tutakutana nao kwenye Makundi ya Champions League Insha Allah.

“Mashabiki wa Simba SC kuleni Sabasaba kwa amani, kuleni Eid vizuri mwenye kuchinja na achinje na baada ya hapo mtafurahi…”

SOMA NA HII  JAMA JAMA..HAWA WAANGOLA WAMEPANIA AISEE...'CHEKI' MPUNGA WATAKAO PEWA WACHEZAJI WAO WAKISHINDA KESHO..