Home Azam FC MBONGO ALIYEKUWA ‘ANAKICHAFUA’ ULAYA ATUA AZAM FC….AMBROUCHE ALIMWACHA STARS…

MBONGO ALIYEKUWA ‘ANAKICHAFUA’ ULAYA ATUA AZAM FC….AMBROUCHE ALIMWACHA STARS…

Habari za Michezo leo

KLABU ya Azam imekamilisha usajili wa kiungo, Adolf Bitegeko aliyekuwa anaichezea timu ya Volsungur IF ya nchini Iceland.

Nyota huyo aliyewahi kukichezea kikosi hicho akiwa akademi amerejea nchini baada ya mkataba wake kumalizika huku akiwa ni miongoni mwa majina yaliyoitwa na Kocha wa Stars, Adel Amrouche kwa ajili ya AFCON inayoendelea Ivory Coast ingawa hakupenya.

Usajili huo ni wa kwanza kwa wachezaji wazawa katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15 huku akiwa ni wa nne baada ya, Mohamed Mustafa kutoka Al-Merrikh, Yeison Fuentes (Leones FC) na mshambuliaji, Franklin Navarro kutokea Cortulua FC.

Mbali na kuichezea Volsungur IF ila timu nyingine alizochezea kiungo huyo ni KR Reykjavik na KeflavĂ­k IF zote za Iceland.

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA KUKIPIGA KUNDI MOJA CAFCL