Home Habari za michezo MOLOKO AFICHUA KILICHOPO NYUMA YA KIWANGO CHAKE…NABI AMTAJA KISINDA…

MOLOKO AFICHUA KILICHOPO NYUMA YA KIWANGO CHAKE…NABI AMTAJA KISINDA…

Nyuma ya kiwango anachokionyesha Ducapel Moloko msimu huu, kinatokana na alamu mbaya iliyokuwepo kwake msimu uliopita, ambapo jina lake lilikuwa linatajwa kuenguliwa, anafunguka usiyoyajua.

Ipo hivi: Moloko amesema kwamba wakati anatua Yanga alipokelewa kwa ukubwa na mashabiki, ingawa hawakuridhika na huduma yake, jambo ambalo msimu huu limempa hamu ya kujituma zaidi.

Wakati anasajiliwa Yanga ilimfanya mbadala ya Tuisila Kisinda ambaye ilimuuza Morocco. “Baada ya kurejea kwa Tuisila kulikuwa na ushindani mkali wa namba, nilikuwa naweza kuanza na kutolewa, baada ya kuona kocha ameanza kuniamini, imenifanya nijitume zaidi kuhakikisha nisipoteze hiyo fursa.

“Sina maana kwamba Kisinda ni mchezaji mbaya, ubora wake ndio unanifanya niwajibike na kuutumia vyema muda ninapokuwepo uwanjani kuisaidia timu kupata matokeo.”

Wakati Moloko akijivunia ubora wake, kocha Nasreddine Nabi alimbadilisha Kisinda kucheza kushoto kutoka winga wa kulia, ambako anaonekana kufiti. Ambapo alicheza dhidi ya Kagera Sugar, Singida Big Stars na Mbeya City na mchango wake ulionekana kwa timu, tofauti na mwanzo.

Wakati huo huo, Joyce Lomalisa na Shomari Kibwana wanampa wakati mgumu, Shaban Djuma kujihakikishia namba kikosini, baada ya mechi tatu akiwa nje, wenzake walionekana kufiti.

Ubora wa Lomalisa ambaye wakati anajiunga Yanga hakuwa na upepo mzuri kwa mashabiki, alianza kukiwasha mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club African ya Sudan, kisha akapangwa tena dhidi ya Kagera Sugar, (Djuma benchi), Mbeya City, Dodoma Jiji na SBS ambazo hakukaa benchi kabisa. Hilo linamfanya kocha Nabi kuamua kuendelea na Lomalisa na Kibwana Shomari kutokana na kitu wanachokitoa kikosini, ikiwa ni mechi ya nne mfululizo wanaanza pamoja.

Mara ya mwisho kwa Djuma Shaban kuonekana uwanjani ilikuwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati raia huyo wa DR Congo akiingia kuchukua nafasi ya Kibwana.

Kitu kingine kilichomfanya Moloko afanye vizuri, awali Yanga ilitaka kumuondoa, lakini ikakata jina la Yacouba Sogne ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha, ila iliendelea kusalia naye kambini akifanya mazoezi.

Mabadiliko mengine ni kwa Kisinda, ambaye urejeo wake Yanga ulikumbana wakati mgumu kwani hakuna ambacho kileleweka kwa mashabiki kutokana na kiwango duni.

Baada ya kuona upande wa kulia unamfanya Kisinda kutokuwa na madhara zaidi, alimbadilisha na kumpeleka kushoto. Hilo limefanyika katika mechi mbili, ambazo dhidi ya Singida Big Stars, wakati akikosa bao kwa krosi ya Mzize, na dhidi ya Mbeya City bao lake likikataliwa.

Nabi alisema: “Kuna kitu watu hawakioni, ana Kisinda hakuja hivi, kuna mabadiliko makubwa kwake, lakini mwangalie kwa sasa. Upande wa kushoto atakuwa na muda mfupi wa kukimbia na kuingia ndani, hili linamfanya kuwa na hatari zaidi, kwa kasi yake ni wazi kwamba anaelekea pauri katika mabadiliko haya.”

SOMA NA HII  BRUNO FERNANDEZ REKODI ZAKE NI BALAA, UTD KUFUZU 16 BORA. BASHIRI MERIDIAN BET