tetesi za usajili Yanga leo
Habari za michezo

MASHINE YA KAZI ILIYOINGIA KWENYE ANGA ZA YANGA YAPAA ULAYA…JAMAA NI FUNDI NA NUSU..

admin February 1, 2024 12:36 pm

Mshambuliaji aliyekuwa akiwindwa na Yanga, Sankara Karamoko amekamilisha uhamisho wa kutua katika Klabu ya Wolfsberger AC ya Austria baada ya kudumu ndani ya Asec Mimosas kwa miaka mitano.

Karamoko (20), ambaye alijiunga na Asec mwaka 2019 akianzia timu ya vijana amekamilisha uhamisho huo baada ya timu hiyo kukubaliana na Wolfsberger AC inayoshiriki Ligi Kuu Astria maarufu kama Ausrian Bundesliga.

Katika msimu huu akiwa na Asec, Karamoko amefanikiwa kuwa kinara wa mabao kwa timu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akikofunga mabao manne.

Wolfsberger AC iko katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi nchini humo ambapo Asec imeeleza kwamba mshambuliaji huyo ameuzwa kwa dau lisiloweza kuwekwa wazi.

Karamoko anakwenda kuungana na mshambuliaji mwenzake wa zamani wa Asec, Karim Konate ambaye naye aliuzwa msimu uliopita kwa klabu ya Redbull Salzburg.

Tayari mshambuliaji huyo ameondoka nchini Ivory Coast akielekea Ausrtia kukamilisha dili hilo ambapo endapo atafuzu vipimo vya afya atasaini mkataba utakaomfanya aishi huo hadi 2027.

Yanga iliweka mitego yake ili kumnasa mchezaji huyo wakati wa dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15, lakini ilishindikana katika ishu ya makubaliano kwa kilichodaiwa kwamba timu yake ilikuwa na mpango wa kumuuza Ulaya.

AFCON YAIPA SIMBA VICHWA VIPYA…YANGA WAJA NA BITI LA KUFA ‘NTU’…. BAADA YA KUANZA BALAA LAKE NA SIMBA….KICHUYA KAIBUKA NA HILI KWA CHASAMBI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply