Home Habari za michezo MASHINE HII YA AFCON KUTUA MSIMBAZI DIRISHA LIJALO….ISHU YAANZA KUSUKWA KIMYA KIMYA…

MASHINE HII YA AFCON KUTUA MSIMBAZI DIRISHA LIJALO….ISHU YAANZA KUSUKWA KIMYA KIMYA…

Habari za Simba leo

Klabu ya Simba SC ina mikakati mizito ya kutengeneza kikosi cha ushindani mkali kwa ajili ya msimu ujao 2024/25, tayari imeunda timu ya maskauti iliyosambazwa nchi tofauti kwenda kuangalia wachezaji wenye viwango vikubwa.

Taarifa zinaeleza kuwa timu ya maskauti itafanya kazi kwa awamu mbili, majina yanayopendekezwa kwa sasa yatachambuliwa Machi na mengine Juni, kisha wataamua nani wamsajili.

Kiongozi huyo amesema timu iliyotumwa kuangalia Wachezaji kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ivory Coast, imepeleka majina mawili mezani.

Wanachezea Mauritania. Nahodha anayecheza kiungo namba nane Bodda Mouhsine na beki wa kati Lamine Ba.

Kiungo Mouhsine anaichezea FC Nouadhibou ya nchi kwao na beki Ba anaitumikia NK Varazdin ya Croatia.

Tulikaa chini na kutafakari ni namna gani tunaweza tukaijenga timu itakayokuwa inanyakua mataji ya ndani na nje, tukaja na mpango mkakati huo, tuliouona utatusaidia na siyo kusajili wachezaji kwa presha, mwishowe wanakuwa hawana msaada.

Pia tutahitaji kuwa na mastaa ambao watakuIwa na levo sawa ya viwango na siyo baadhi vinakuwa juu, wanapopata shida timu inakuwa inayumba.”

Hata hivyo, wanachokifanya Simba SC ni moja ya utaratibu wa kawaida kwa timu nyingi zilizoendelea kwani Sevilla wakati inamwajiri Ramon Rodriguez Verdejo Monchi kama mkurugenzi wao wa michezo mwaka 2000, alianzisha kitengo cha maskauti waliopatikana nchi mbalimbali duniani.

SOMA NA HII  JEMEDARI SAIDI:- SUALA LA CHAMA, SIMBA WALITUDANGANYA....?..