Habari za Azam
Azam FC

KUELEKEA MECHI YAO NA SIMBA….KOCHA AZAM FC AANZA KUJIPA SABABU….

admin February 5, 2024 12:10 pm

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema licha ya kutojua hadi sasa uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaopigwa Februari 9, lakini haijawatoka mchezoni na badala yake wanaendelea na maandalizi.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini kutokana na ubora wa vikosi hivyo, awali ulipangwa kuchezwa Januari Mosi, mwaka huu, lakini ulishindwa kuchezwa kutokana na ratiba kubana ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 pamoja na michuano ya Afcon ambayo Taifa Stars ilishiriki.

“Tunaendelea kujipanga vizuri, ila suala la wapi mchezo utachezwa kwetu halitusumbui kwa sababu ninachoamini maandalizi bora siku zote ndio yanayokupa matokeo chanya. Tuko tayari kupambana tukitambua ni mchezo mgumu,” alisema kocha huyo raia wa Senegal.

Dabo aliongeza kuwa wakati wapinzani wao wanaendelea kucheza michezo ya viporo iliyobaki, wao pia wanatafuta angalau mechi mbili za kirafiki zitakazowaweka wachezaji wa kikosi hicho katika ushindani mzuri kabla ya kukutana na Simba.

“Tayari tuna mchezo na Mafunzo ya Zanzibar na baada ya hapo tunaangalia kama Jumatatu au Jumanne tutapata mwingine zaidi ili kujiweka fiti. Hatujiandai kwa ajili ya Simba pekee bali ni kwa michezo yote ya kiushindani iliyopo huko mbeleni.” Mchezo wa mwisho wa ligi baina ya timu hizo ulipigwa Februari 21, mwaka jana ambapo zilifungana bao 1-1

DIARRA DAH….INONGA NI BALAAHA TUPU HUKO…PA JOBE ATULIZA ‘MUKARI’ SIMBA SC.. KISA PHIRI NA BALEKE….STRAIKA MPYA SIMBA KAIBUKA NA ‘DONGO’ HILI KWAO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply