Habari za Yanga leo
Habari za michezo

BARESI:- TUTATUMIA MBINU ZA IHEFU KUMALIZANA NA YANGA MAPEMA…

admin February 8, 2024 11:38 am

Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah Baresi’ amesema watatumia mbinu za Ihefu FC kuwafunga Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans.

Mashujaa inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, leo Alhamis (Februari 08) itakuwa mgeni wa Young Africans katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam Kocha huyo amesema wanalazimika kutumia mbinu zitakazowapa ushindi ili kujiondoa kwenye nafasi mbaya waliyopo sasa.

“Ukweli tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya vinara na mabingwa watetezi lakini tumepanga kutumia mbinu za Ihefu ambayo ndiyo timu pekee iliyoifunga Young Africans msimu huu,” amesema Baresi.

Kocha huyo kutoka visiwani Zanzibar ambaye timu yake ilipoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba SC, amesema anaridhishwa na upambanaji wa kikosi chake ambacho kina wachezaji waliosajiliwa kwenye dírisha dogo na anaamini nafasi ya kufanya vizuri kwao ni kubwa.

Amesema kinachowasumbua kwa sasa ni kupata ushindi wa kwanza utakaowajengea kujiamini na wamepanga kulifanya hilo.

Baadhi ya nyota waliosajiliwa na Mashujaa kwenye dirisha dogo ni pamoja na Reliant Lusajo, Balama Mapinduzi, Eric Johora, Zuber Dabi, Ibrahim Ame na Abrahaman Mussa.

PAMOJA NA KUFUNGA GOLI LA USHINDI JUZI….MUDATHIR KAIBUKA NA HILI JIPYA YANGA…. RAIS SAMIA ‘ATIA MKONO’ UWANJA WA YANGA JANGWANI….BENKI YA DUNIA KUMWAGA MABILIONI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply