Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YAO YA CAF…SIMBA WAMTANGULIZA KRAMO ‘KUISNICHI’ ASEC MIMOSAS…

KUELEKEA MECHI YAO YA CAF…SIMBA WAMTANGULIZA KRAMO ‘KUISNICHI’ ASEC MIMOSAS…

Habari za Simba leo

KIUNGO wa Simba, Aubin Kramo na mratibu wa Simba, Abbas Ally, wametangulia na kwenda nchini Ivory Coast kuweka mazingira ya ushindi kwa timu yao itakapocheza dhidi ya Asec Mimosas ya nchini humo.

Kuondoka kwa Kramo kufanya kazi hiyo ya kuweka mazingira sana kutokana na kwamba atakuwa nyumbani kwao, pia akiwa ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Ivory Coast, ni kama ndiye msuka ramani ya vita katika kecho hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Kramo na kigogo huyo wanaondoka leo kwa ajili ya maandalizi ya Simba itakapofikia pamoja na kuweka mikakati mingine ya ushindi.

Simba wanatarajia kuondoka Jumatatu au Jumamne kuelekea nchini humo, kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ambapo watacheza kwenye moja ya uwanja uliotumika kwenye mashindano ya AFCON, 2023, uwanja wa Felix, Houphouel- Boign, Februari 23, mwaka huu.

Taarifa za uhakika kuwa Kramo atakuwa sehemu ya msafara wa Simba ambao watatangulia kwenda nchini humo kwa sababu nyota huyo anatoka nchini humo na kufahamu sehemu zote na pamoja na kuifahamu vema Asec Mimosas.

“Kramo atakuwa sehemu ya watu wanaokwenda nchini humo kabla ya timu kuondoka, nyota huyo anafahamu sehemu zote za nchini humo, pamoja na kuifahamu vizuri wapinzani wao Ivory Coast,” amesema chanzo hicho.

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amesema baada ya kukamilika kwa mchezo na JKT Tanzania alikutana na wachezaji wake kuzungumza na kuweka mipango ya ushindi kuelekea mchezo wao dhidi Asec Mimosas kuhakikisha anavuna pointi muhimu.

Amesema kuna taarifa muhimu amepokea kuhusu wapinzania wao ikiwemo mbinu za kifundi ikiwemo ubora na madhaifu yao hali ambayo wanafanyia kazi kuhakikisha wanakuwa imara safu ya ulinzi na ushambuliaji.

“Ni mechi muhimu kwetu kushinda, tumeanza kufanyia kazi ubora wa Asec Mimosas, lakini pia kusahihisha makosa tuliyoyafanya katika michezo iliyopita, tutapata muda wa kufanya maandalizi mazuri na kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo wetu ujao,” amesema kocha huyo.

Ameeleza kuwa mikakati yao ni kuona wanaenda kupambana kutafuta matokeo chanya ugenini dhidi ya Asec Mimosas, mchezo mgumu kwa sababu wapinzani wako nyumbani na wanahitaji kutumia vizuri.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI