Home Habari za michezo FT: YANGA 5-0 POLISI TZ…..GUEDE AFUTA GUNDU KIBABE….G5 ZA GAMONDI BADO...

FT: YANGA 5-0 POLISI TZ…..GUEDE AFUTA GUNDU KIBABE….G5 ZA GAMONDI BADO WAARABU TU…

Habari za Yanga leo

Nyota wa kimataifa wa Ivory Coast aliyesajiliwa dirusha dogo la usajili, Joseph Guede ameifungia Yanga mabao mawili ikiichapa Polisi Tanzania mabao 5-0, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Kombe la Azam Sport Federation Cup (ASFC), umeshuhudia Yanga ikiendeleza moto wake wa kuzichapa timu zinazokutana nazo mabao matano, ukiwa ni ushindi wa pili wa idadi hiyo ya mabao kwenye michuano hii baada ya awali kuifunga Hausung mabao 5-1 kwenye mchezo wa hatua ya pili.

Guede amefunga mara mbili mabao yake ya kwanza ndani ya timu hiyo kwenye dakika za 13 na 45+1 yote akiyafunga kwa kichwa akitumia krosi za winga Augustine Okrah.

Winga Farid Mussa aliipa Yanga bao la pili dakika ya 32 akitumia krosi ya kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz KI na kuifanya timu yao kwenda mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao hayo 3-0.

Kipindi cha pili Yanga ilipata bao la nne kupitia mshambuliaji wake Clement Mzize akimalizia krosi ya beki wake wa kulia Kibwana Shomari dakika ya 82 kabla ya kiungo mshambuliaji, Shekhan Khamis kumalizia msumari wa tano kwa penalti baada ya Mzize kuangushwa akiwa anaenda kufunga.

Bao hilo la Mzize limemfanya kufikisha manne msimu huu baada ya awali kupiga mabao matatu Hat trick kwenye mchezo wa hatua ya pili.

Yanga sasa inajiandaq na mchezo wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi Februari 24, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na itaikaribisha CR Belouizdad iliyolingana nayo pointi zikiwa na tano.

Katika mchezo huo, Yanga iliwakosa nyota wake Djigui Diarra, Dickson Job, Nickson Kibabage, mudathir Yahya, Kennedy Musonda khalid Aucho na pacome Zouzoua, huku Kocha Miguel Gamondi akiwatumia wachezaji ambao walikosa baadhi ya michezo akiwamo Aziz Ki na Bakari Mwamnyeto na kuwapa nafasi baadhi ya nyota wake ili kuwarudishia ufiti kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA SIMBA WALIVYOFINYANGWA JANA...IBENGE AINGIA UBARIDI KUKUTANA NA YANGA CAF...