Uncategorized

DUBE ATAKATA AZAM FC IKIPIGA 4G

admin October 13, 2020 4:47 am

 


PRINCE Dube, jana Oktoba 12 alikoingoza kikosi chake cha Azam FC kuubuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. 


Bao la Kwanza kwa Azam FC lilipachikwa na kiungo Mudathir Yahya dakika ya 24 dakika ya 43 Dube ambaye alifunga mabao mawili alipachika bao lake la Kwanza Kwenye mchezo huo kwa mkwaju wa penalti na kuifanya Azam FC kuwa mbele kwa mabao 2-0.


Bao lake la pili alipachika dakika ya 44 na kufanya Azam FC kuwa mbele kwa mabao 3-0 mpaka muda wa mapumziko na Fountain Gate ambao wanashiriki Ligi Daraja la Kwanza walikwama kupata bao la kufuta machozi.


Msumari wa mwisho ulipachikwa na Kader dakika ya 49 na kuipa ushindi timu yake hiyo Uwanja wa Azam Complex.

BEKI MZAWA DAVID LUHENDE AINGIA ANGA ZA SIMBA NA YANGA KANTE ANATAKA KUONDOKA CHELSEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply