Home Habari za michezo ALIYEWASIMAMIA YANGA KUIMALIZA MAZEMBE…APEWA MECHI YA ASEC vs SIMBA LEO…

ALIYEWASIMAMIA YANGA KUIMALIZA MAZEMBE…APEWA MECHI YA ASEC vs SIMBA LEO…

Habari za Simba leo

Mwamuzi Lahlou Benbraham, 37, kutoka Algeria ambaye alichezesha msimu uliopita mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga ndiye aliyepewa jukumu la kuiamua mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya ASEC Mimosas dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Abidjan kesho.

Hii itakuwa mara ya pili kwa mwamuzi huyo, kuchezesha mechi ambazo zinahusisha timu za Tanzania tena mechi zote zikiwa ugenini, ile ya Yanga, Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Farid Mussa huku zikimwagwa kadi tano za njano na nyekundu moja ambayo alionyeshwa, Alex Ng’onga wa Mazembe.

Takwimu zinaonyesha mwamuzi huyo ametoa kadi za njano 22 na nyekundu moja msimu huu ndani ya michezo mitano tu aliyochezesha kwenye mechi za Ligi Kuu Algeria ambayo ni maarufu kama Ligue Professionnelle 1.

Mechi aliyomwaga kadi nyingi zaidi ilikuwa Desemba 15 mwaka jana, 2023 kati ya MC El Bayadh dhidi ya USM Alger, alitoa kadi saba za njano kwa upande wa ligi ya ndani huku kimataifa akionekana kuwa balaa zaidi.

Kimataifa Benbraham ametoa kadi 19 kwenye michezo mitatu iliyopita huku akigawa nyekundu kwenye kila mchezo, hivyo nyota wa Simba kama vile Sadio Kanoute wanatakiwa kuwa macho vinginevyo wanaweza kugharimu mipango ya timu yao kwenye mchezo huo.

Mara yake ya mwisho kucheza michuano ya CAF ndio ilikuwa mechi kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga ambayo ilitoa kadi tano za njano.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MZIKI WA MUSONDA...STRAIKA SIMBA AWAPA YANGA UBINGWA MSIMU HUU...