Home Habari za michezo BAADA YA KUBANWA IVORY COAST JANA….SIMBA KUJA KIVINGINE ‘GAME’ NA JWANENG…

BAADA YA KUBANWA IVORY COAST JANA….SIMBA KUJA KIVINGINE ‘GAME’ NA JWANENG…

Habari za Simba leo

UONGOZI wa benchi la ufundi Simba umesema kuna mambo mawili ambayo wanatakiwa kuyafanya katika mchezo wa mwisho wa kundi lao la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ikiwemo kulipa kisasi na kusaka ushindi utakaowapeleka kucheza robo fainali.

Simba jana walicheza mchezo wa wa hatua ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya ASEC Mimosas uliopigwa Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny umemalizika kwa suluhu, nchini Ivory Coast.

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema mechi haikuwa rahisi walihitaji pointi tatu lakini wamepata moja, wamefanikiwa katika malengo yao.

Amesema kubwa ni kuwazuia Asec Mimosas wasipate bao hilo wamefanikiwa, baada ya mechi hiyo jana wameanza maandalizi kuelekea mechi ijayo dhidi ya Jwaneng Galaxy kuhakikisha wanapata ushindi.

“Jana tumeanza maandalizi kuelekea mchezo wetu wa mwisho ambao ni fainali, kuna mambo mawili katika mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy kutafuta ushindi utakaotupeleka hatua ya robo fainali na kulipa kisasi.

Hii haitakuwa mechi ya kawaida bali ni fainali kwa Simba kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kwenda robo fainali kwa kumfunga mpinzani wetu huyo,” amesema Matola.

Ameeleza kuwa hawataki kurudia makosa ya miaka iliyopita kwa kupoteza nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy, hali ambayo walianza maandalizi mapema baada ya dakika 90 kukamilika kwa mechi ya juzi na Asec Mimosas.

Akizungumzia mchezo wa jana, amesema ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

“Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi kwa kuliandama lango la Asec Mimosas, dakika ya 46 Sadio Kanoute alipoteza nafasi ya wazi baada ya kumzidi ujanja mlinda mlango lakini shuti lake lilitoka pembeni kidogo.

Tuliendelea kutengeneza nafasi huku wenyeji nao wakija golini kwetu mara kadhaa lakini hakuna aliyeweza kutumia nafasi zilizopatikana, tukalazimika kuzuia dakika za mwishoni ili kutowapa nafasi ya kutufunga ikiwa malengo yetu kutafuta pointi ugenini na tumefanikiwa,” amesema Matola.

Naye kiungo wa Simba, Clatous Chama amesema mechi haikuwa rahisi kwa sababu wapinzanu walikuwa nyumbani na walihitaji kupata matokeo uwanja wa nyumbani, mioango yao ikiwa ni kurejea Tanzania na pointi moja.

“Hatua moja muhimu kupata pointi moja mbali na nyumbani, wakati wa kurejea nyumbani (Tanzania) na kumaliza kile tulichoanza,” amesema Chama.

Amesema wanarejea nyumbani kupambana kufuta ushindi katika mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy, fainali kuhakikisha wanapata ushindi na kutorudia makosa ambayo yaliyofanyika katika mechi ya nyuma dhidi ya mpinzani wao.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amesema anawapongeza wachezaji kwa kupambana na kuvuna pointi moja muhimu dhidi ya Asec Mimosas .

“Mechi ya mwisho ya nyumbani Tanzania itakuwa zaidi ya fainali , kila shabiki ajiamdae kwa mchezo huu muhimu,” amesema Try Again.

Matokeo ya jana yanawafanya Simba kuendelea kubaki nafasi ya pili tukiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi tano.

SOMA NA HII  YANGA YATUMA SALAMU GEITA GOLD