Habari za Yanga SC
Habari za michezo

KWA TAKWIMU HIZI….SIO AJABU KWA PACOME ALIVYOOMBWA JEZI NA MCHEZAJI WA CR BELOUIZDAD..

admin February 27, 2024 2:33 pm

Kitendo cha mshambuliaji wa CR Belouizdad, Lamin Jallow raia wa gambia kumfuata Pacome Zouzoua baada ya Mchezo na kumuomba jezi kinatosha kuelezea kazi aliyoifanya.

Pacome ndiye mchezaji aliyeugusa mpira (Touches mara 65) mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote juzi pale kiwanjani.

Pacome ndiye mchezaji aliyetengeneza nafasi nyingi ambapo kati ya nafasi 10 walizotenegenza Yanga, nafasi tano alitengeneza Pacome.

Pacome alipiga shuti moja golini na hakupiga shuti nje ya lango. Alishika mpira ndani ya boksi la CRB mara 8 akikokota mpira mara 4 na kufanikiwa.

Pacome alikipa pasi 9 sehemu ya robo tatu kwa mpinzani, akipiga pia mipira mirefu 7 na hajapoteza mpira wowote mguuni kwake.

Hajaishia hapo tu, Pacome alisaidia kwenye ulinzi akiondoa hatari moja kwa kichwa, alifanya inteception mara moja na alipokonya mipira mara 11.

Kwenye mipira ya juu ya kugombania alishinda mitano kati ya 9 na alifanyiwa faulo mara moja lakini hakufanya faulo yoyote.

Aziz Ki alitengeneza nafasi nne na Mudathir alitengeneza nafasi moja.

Katika michezo (5) kwenye group stage CAF-CL, Pacome hajahusika kwenye goli katika mchezo mmoja pekee.

◉ ⚠️ vs CR Belouizdad (0-3)
◉ ⚽ vs Al-Ahly (1-1)
◉ ⚽ vs Medeama (1-1)
◉ ⚽ vs Medeama (3-0)
◉ Assist vs CR Belouizdad (4-0)

Takwimu za mchezo;
Yanga …. vs …. Belouizdad
____________
16 ………… Shots ……………….. 10
8 …….. Shots on target ………… 2
54% …… Possession ………….. 46%
459 ………. Passes …………….. 397
83% ….. Pass accuracy ………. 79%
2 …………… Corner ………………..3

Note : Zile mbizi alizompigisha golikipa wa CR Belouizdad pamoja na ile Assist kwa Musonda ni vielezi tu kuhusu Umahiri wake na kwa nini wanamuita Professor.

WAKATI UPANDE WA PILI NI VICHEKO TUPU…BENCHIKHA KATAZAMA WEE..KISHA AKASEMA HILI… BAADA YA KUIFANIKISHIA KUTINGA ROBO FAINAL CAF….GSM KABAKI NA DENI HILI TU KWA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply